UKWELI MCHUNGU..Kiapo cha Baraza la Mawaziri Ndio Sababu ya Ukimya wa Lowassa Kwenye Sakata la Richmond.
BLOG NO 1 TANZANIA !! Lowassa yuko kimya kabisa wala hazungumzii mambo yalivyokuwa ndani ya Serikali tangu atoke kwenye Uwaziri Mkuu ambao alijiuzulu mwaka 2008. Kuna baadhi ya watu wanautafsiri ukimya wa Lowassa kama ni woga ama kukiri kwamba alishiriki kwenye “Ufisadi” wa Richmond. Lakini Lowassa alikuwa ni Waziri Mkuu na kwa kawaida Waziri Mkuu hula kiapo cha uaminifu na cha kutunza siri za Baraza la Mawaziri ambacho kipo Kisheria. Lakini pia kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 52 ambayo inataja majukumu na mipaka ya kazi za Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Rais aliyeko Madarakani. Ukisoma pia Ibara ya 35 (i) wafanyakazi wote wa serikali wanafanya kazi kwa niaba ya Rais. Jambo la Richmond kupewa Tenda ya kuleta Jenereta za Kufua Umeme lilianzia kwenye Baraza l...