Posts

HII NI DHARAU KWA RAIS SIO UHURU WA KUONGEA ALICHOKIFANYA HUYU KIJANA

Image
Kijana ambae blog hii imefanya uchunguzi na kugundua anatumia jina la Laude Frank Mbwesi amemkosea adabu Rais wa jamhuri ya wananchi wa Tanzania kwa kujibu Twitter ya Rais bila adabu kuna aina ya kuongea na mkuu wa nchi na kuna njia mbalimbali za kufikisha ujumbe kwa Raisi sio hatua hii ambayo huyu

INASIKITISHA: BOMU LILISHINDWA KUNYOFOA UHAI WA MTOTO HUYU LAKINI AJALI YA JUZI IKACHUKUA UHAI WA MTOTO HUYU

Image
MTOTO aliyejeruhiwa kwa bomu lililorushwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti miaka minne iliyopita, Arnold Alex amefariki dunia kwa ajali ya basi la Shule ya Awali na Msingi ya Lucky Vincent juzi.

HALI YACHAFUKA MSIBANI MKUU WA MKOA WA ARUSHA NA LEMA WACHAFUA HALI YA HEWA SOMA KWA UNDANI AIBU HII

Image
Anaandika Mhe.Godbless Lema.! ___________________________________________ Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali. Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole. Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea, nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mhe.Ole Nasha, nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais hasingeweza kukubaliana na ujinga huu. Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani, jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambi rambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika nailionekana dhairi kuwa sitakiwi kabosa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na m...

TBC YASHAMBULIWA KILA KONA ,KUTOKANA NA KUSHINDWA KURUSHA LIVE KUAGWA KWA MIILI ARUSHA.

Image
Hakika katika televishion iliyowashangaza watanzania wengi ni TBC,hii inatokana na kushindwa kuonyesha live tukio kubwa la msiba wa wanafunzi 32 waliofariki kwa kupata ajali ya gari.Huku baadhi ya televisheni binafsi ka clouds zikitoa taarifa kwa kina na ukaribu wakionyesha kiguswa sana na tukio hilo.Cha ajabu televisheni ya Taifa ambayo ndo ingekuwa karibu sana na tukio hilo.Mitandaoni watu wamelaani sana kitendo cha tbc kutofanya coverage ya moja kwa moja juu ya tukio hili la huzuni kwa taifa.

TAZAMA LIVE: KINACHO ENDELEA ARUSHA KWENYE KUAGA MIILI YA WANAFUNZI 38 WALIO KUFA KARATU

Image
BONYEZA HAPA KUSIKILIZA KWENYE REDIO 24 RADIO

Makamu wa Rais Yupo Jijini Arusha kuongoza maombolezo ya watu 36 waliofariki

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliwasili mjini Arusha jana jioni  ambapo leo  ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu wawili pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali juzi tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha. Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule  iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu. Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hii

Ajali Lusanga Muhez: Watu 4 Wafariki Dunia, 15 Wajeruhiwa

Image
Watu 4 wamefariki na 15 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugonga lori katika Kijiji cha Lusanga Muheza. Majeruhi wapo Hospitali Teule ya Muheza. Bado tunafatilia Habari kwa kina