Watu 26 wauawa kanisani Texas Marekani
Askari na wafanyakazi wa dharura wakiwa katika eneo la mauaji katika kanisa la First Baptist huko Sutherland Springs, Texas, Nov. 5, 2017. Mtu mmoja anayeaminika kuwa mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Marekani aitwaye Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26 ameshambulia watu kwenye kanisa moja karibu na San Anrtonio jumapili asubuhi na kuuwa watu 26 na kujeruhi wengine wasiopungua 20. Walioathirika katika shambulio hilo la kanisani kwa silaha nzito za risasi za mauaji ya halaiki ni kati ya umri wa miaka 5 hadi 72. Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na bado haijulikani sababu ya kuchukua hatua hiyo. Wachunguzi kutoka idara ya makosa ya jinai FBI na idara ya usimamizi wa vilevi, tumbaku na silaha wako Sutherland Springs Texas kiasi cha kilometa 50 kutoka San Antonio. Rais Donald Trump ameita mauaji hayo kitendo cha kikatili na kutoa wito wa maombi. Rais anafuatilia hali ilivyo akiwa Japan kituo chake cha kwanza katika ziara ya n...