Posts

Showing posts with the label Michezo Kitaifa

MASHABIKI WA MBAO NA SIMBA HEBU MSIKIENI MANJI ANACHOSEMA!! HUYU SI MTU MZURI HATA KIDOGO TENA HAFAI !!!

Image
YANGA ni kama vile tayari imeshawanyamazisha watani wao Simba kwa hatua ya kutangaza ubingwa rasmi Jumanne lakini kuelekea kumaliza mechi mbili za mwisho, mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji amewatia mzuka wachezaji akiwapa ahadi nono. Taarifa kutoka ndani ya kikosi cha Yanga ni kwamba Manji amewataka wachezaji wa timu hiyo kupambana kwa nguvu katika kumalizia Ligi huku akiwataka kuhakikisha wanashinda mpaka mchezo wa mwisho dhidi ya Mbao,  kesho Jumamosi Mei 20 pale CCM Kirumba jijini Mwanza. Katika taarifa yake hiyo, Manji anaelezwa amewapa ahadi kubwa wachezaji wa timu hiyo kwamba anataka kumaliza tatizo lao la mishahara huku akiwapa ahadi nyingine ambayo imewatia mzuka zaidi. “Mwenyekiti yupo pamoja na timu ila hataki kufanya mambo yake kwa mazoea, ameongea na wachezaji na hivi karibuni amewaambia hakuna kitu kitakachopotea katika haki zao, mishahara yao watapatiwa na mambo yote,” alisema bosi huyo. “Unajua wachezaji wetu walivyo kama wasingekuwa wamepewa pochi halisi ya m...

KABURU ATHIBITISHA MO, POPPE HAWANA KINYONGO TENA... asema sasa ni "Nguvu Moja" kuziua Mwadui FC na Mbao

Image
KAULI mbiu ya klabu ya Simba ni maeneo mawili mazito lakini yanayoonekana ni yenye maana kubwa katika maisha ya watu wanaotamani kupata mafanikio, “Nguvu Moja.” Maneno haya yametumika katika vikao viwili tofauti ndani ya siku tatu, kikao kimoja kikiwa ni cha wajumbe wa Kamati ya Utendaji dhidi wa wajumbe wenzao, kapteni Zakaria Hans Poppe ambaye alikuwa ametangaza kujiuzulu nafsi zake zote katika klabu hiyo. Kamanda huyo wa zamani wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alikuwa amekerwa na kitendo cha viongozi wenzake katika Simba kuingia mkataba wenye thamani ya sh bil 4.9 na kampuni ya Sportpesa ya Kenya. Inadaiwa kuwa Hans Poppe alikuwa akipinga Simba kuingia mkataba huo bila kuujadili kwa kina, lakini pia bila kumshirikisha mwanachama mwenzao anayeisaidia Simba kwa hali na mali, “Mohammed Dewji” “MO”. Lakini kikao cha siku moja baina ya viongozi na Poppe kikamaliza udhia na mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili akatengua uamuzi wake na kurejea kazini. Baada ya kikao hicho ...

BALAA KUBWA MSIMBAZI: MO ATAKA SIMBA IMLIPE BILIONI 1.4 PATA HABARI KWA UNDANI HAPA!!

Image
Siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ anataka kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 za Tanzania kutokana na viongozi wa Simba kukiuka makubaliano.

MSUVA: NITAHAKIKISHA YANGA INATETEA UBINGWA WA LIGI KUU BARA KWANZA

Image
KINARA wa ufungaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amesema kuwa kipaumbele kikubwa kwake ni kuhakikisha Yanga inatetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na sio kuwaza mafanikio binafsi. Msuva ambaye ni kinara wa ufungaji katika klabu yake ya Yanga ambapo kabla ya mchezo na Prison alikuwa na mabao 12

HABARI MBAYA!!! JENGO LA KLABU YA YANGA KUPIGWA MNADA

Image
JENGO la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.

Ally Yanga apata kipigo kutoka kwa mashabiki wa mwanza kwa tuhuma za ushirikina

Image
Shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga amekutana na kipigo kikali kutoka kwa mashabiki walioelezwa ni wa Simba wanaoiunga mkono Mbao FC.

SERENGETI BOYS WAICHANA CHANA CAMEROON KWAO!!

Image
Yaoundé,Cameroon. TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,Serengeti Boys imeendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi zake za kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa michuano ya vijana ya AFCON baada ya jana Jumapili usiku kuifunga timu ya vijana wenzao ya Cameroon bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Ahmadou Ahijo, mjini Yaounde. Bao la ushindi la Serengeti Boys limefungwa na Ally Nganzi katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza. Serengeti Boys itajitupa tena uwanjani Mei 3 mwaka huu kurudiana na wenyeji wao Cameroon katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu kabla ya Mei 7 kuelekea nchini Gabon tayari kwa michuano ya AFCON. Serengeti Boys iko kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

NILETEENI "KIPRE TCHETCHE" MUONE YANGA ITAKAVYOTISHAA!!

Image
BEKI wa Yanga, Vincent Bossou, amesema mshambuliaji wa zamani wa Azam, Kipre Tchetche, ni muhimu katika kikosi hicho. Tchetche ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu Al-Nahda-Buraimi ya  Oman, ametajwa ni mshambuliaji pekee anayeweza kuisaidia Yanga.

DIAMOND NA ALIKIBA WAGOMA KUIMBA WIMBO WA SERENGETI BOYS

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** *********************

HEBU KISOME !! ALICHOKIONGEA FAKHI WA KAGERA SUGAR KUHUSU SIMBA

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** ********************* Hatimaye mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi amefuguka ya moyoni na kusema anamshukuru Mungu suala lake limeweza kuisha huku akidai furaha na amani kurejea katika familia yake kutokana na kurudishiwa ushindi wao kutoka kwa timu ya Simba Fakhi amesema hayo baada kuisha lile vuguvugu la muda mrefu lililokuwa linamuandama kutoka kwa wapinzani wao Simba SC wakidai kuchezeshwa  katika mechi akiwa na kadi tatu za njano na kupelekea kupokwa matokeo yao hapo awali.  "Namshukuru Mungu suala hili limekwisha vizuri....kwa timu yangu kurudushiwa point zake najiona mwenye furaha, amani imerejea familia yangu nayo imetulia kwani suala hili liliwaweka kwenye 'tention' kubwa. Alisema mchezaji huyo Vile vile Fakhi amewashukuru viongozi wake wa Kagera Sugar pamoja na wachezaji wenzake kwa sapoti waliyokuwa wanampa muda wote huku akisisitizia kuwa nguvu yote sasa...

SIMBA MEZA YAVUNJIKA!! POINT ZARUDISHWA KAGERA SUGAR FC

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** ********************* Hatimaye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipokonya pointi tatu Simba SC, ilizokuwa imepewa kutoka kwa Klabu ya Kagera Sugar. Awali, Simba ilikuwa imepewa ushindi wa mezani wa pointi tatu na magoli matatu dhidi ya Kagera Sugar, baada ya mchezo wake na timu hiyo ya mkoani Kagera kumalizika ikiwa imepigwa magoli 2-1. Ushindi huo wa mezani ulitokana na malalamiko kuwa Kagera Sugar ilimchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano, hivyo hakuwa na sifa za kushiriki mchezo huo kwa mujibu wa kanuni na sheria za Soka. Akitangaza uamuzi wa kurejesha matokeo ya awali ya uwanjani leo katika ukumbi wa Habari wa TFF, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Selestin Mwesigwa alisema kuwa sababu zilizopelekea Kamati kuchukua uamuzi huo, ni pamoja na kucheleweshwa kwa malalamiko ya Simba SC dhidi ya Ka...

Alicho kiandika JERRY MURRO BAADA YA MANARA KUFUNGIWA

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** *********************

Alichokiandika HAJI MANARA usiku huu juu ya kufungiwa kwake

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** *********************

simba yashinda mpira wa mezani yapewa pointi 3 za kagera sugar

Image
                                                   BLOG NO 1 TANZANIA !! Hatimaye kamati iliyokaa leo imebaini Timu ya kagera Sugar ilimchezesha mchezaji wake Muhamad Fakhy hukunakiwa na kadi 3 za njano ambalo ni kosa kisheria.sasa Timu ya simba imepatiwa point 3 na magoli mawili na hivyo kupelekea Kagera Sugar kupokwa point 3 na magoli 2.Katika mchezo huo Simba ilifungwa goli 2-1 na Kagera Sugar

machinga:Yanga wana kibarua kigumu Algeria

Image
                                                     BLOG NO 1 TANZANIA !!

Malinzi:Njooni muone tunavyomchinja Mnyama leo jioni CCM Kirumba

Image
                                          BLOG NO 1 TANZANIA !! Mwanza,Tanzania. MSEMAJI wa Mbao FC, Chrisant Malinzi amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao leo jioni wa ligi kuu bara kujionea jinsi wanavyomchinja Mnyama,Simba SC pale kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba. Malinzi amesema wamejiandaa vizuri na hawawezi kuiogopa Simba SC kwa jina wala historia yake.Ameongeza kuwa waliutazama mchezo uliopita wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar na wakabaini mapungufu kadhaa ambayo watayatumia kuondoka na pointi zote tatu kwenye mchezo wa leo. “Tumejiandaa vizuri na tutafanya vizuri na kushinda kwani vijana wako tayari na hatuna hofu na suala la wao kuwafunga Simba SC.Mashabiki wetu waje kwa wingi.Tumejiandaa mwezi mzima kwa ajili ya mchezo huu na michezo yetu yote iliyobaki ya ligi kuu bara amesema Malinzi.

Akilimali asema Chirwa ameshindikana

Image
                                                BLOG NO 1 TANZANIA !! Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema straika wa timu hiyo, Mzambia, Obrey Chirwa, ameshindikana kwa jinsi anavyowanyanyasa wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara. Mzee Akilimali ametoa kauli hiyo baada ya juzi Jumamosi Chirwa kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar. Awali, wakati Chirwa aliposajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, Mzee Akilimali alikosa imani na Mzambia huyo na kuanza kumuona ‘galasa’ baada ya kuanza vibaya katika ligi. Lakini baada ya kuanza kuzifumania nyavu na sasa akifikisha mabao tisa, Akilimali amekuwa akimsifia kila kukicha na kusema ni miongoni mwa washambuliaji hatari na walioshindikana katika Ligi ya Bongo. Mzee Aki...

Serengeti Boys yaifunga Burundi mbili bila

Image
                                            BLOG NO 1 TANZANIA !!                             Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeifunga wenzao wa Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa marudia baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Alhamis ya wiki hii na kushuhudia Serengeti Boys ikishinda tatu kwa bila na Leo tumeshuhudia Serengeti Boys imeshinda kwa magoli mawili kwa bila. Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Issa Abdi Makamba Kwa faulo ya moja kwa moja na goli la pili likifungwa na Ibrahim Ali kwa kuunganisha mpila ulipigwa na Captain Issa Makamba na kuzaa goli la pili. Serengeti boys itacheza mchezo mwingine wa kujipima nguvu na wenzao wa Ghana Tarehe tatu mwezi huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Serengeti Boys mwendo ni Gabon Mpaka kombe la Dunia ...

Mbwana Samatta ageuka lulu Ujerumani

Image
                                                 BLOG NO 1 TANZANIA !!                             Mshambuliaji wa timu ya KRC Genk inayoshiliki ligi kuu nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta ametajwa kwenye mipango ya timu kubwa tatu za nchini Ujerumani. Vilabu hivyo ni Wolfburg, Humburger na Borrusia Monchenglabach vyote vinataka kumsajili Samatta anayekadiriwa kuwa na thamani ya Euro million 10. Samatta mwenye mkataba na KRC Genk hadi 2020 ameripotiwa kuwa ataruhusiwa kuondoka Luminus Arena iwapo tu  vilabu hivyo vya Ujerumani vitakubali kutoa kiasi hicho cha fedha. Samatta alijiunga na KRC Genk Januari 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo ilimsajili kutoka Simba SC ya Dar Es Salaam,Tanzania.

Hakuna zawadi ya mpira kwa mchezaji atakayefunga hat-trick

Image
                                                    BLOG NO 1 TANZANIA !! Unguja. CHAMA cha soka cha Zanzibar,ZFA kimetangaza kuondoa zawadi ya mpira kwa mchezaji atayefunga mabao matatu ( Hat-trick) dhidi ya klabu ya Kimbuka FC inayoshiriki ligi kuu ya visiwani humo. Akitoa taarifa hiyo msemaji wa ZFA,Ally Bakari Cheupe amesema wameamua kuchukua uwamuzi huo baada ya Kimbuka FC kushindwa kuonyesha upinzani wowote kwenye ligi hiyo na badala yake kuonekana ipo tu kwa ajili ya kukamilisha ratiba na siyo kushindana. Tangu kuanza kwa ligi kuu Zanzibar Octoba 27 mwaka jana,Kimbuka FC iliyoko kanda ya Unguja imekuwa ikiburuza mkia kwani mpaka sasa imecheza michezo 27 na kuambulia pointi 5 pekee.