BALAA KUBWA MSIMBAZI: MO ATAKA SIMBA IMLIPE BILIONI 1.4 PATA HABARI KWA UNDANI HAPA!!
Jana Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu Bw. Evans Aveva, ulisaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
MO anataka kulipwa pesa zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji wa Simba tangu mwaka jana baada ya kubaini kuwa Simba imeingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.
MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.
Comments
Post a Comment