Posts

Showing posts with the label Habari kimataifa

Watu 26 wauawa kanisani Texas Marekani

Image
Askari na wafanyakazi wa dharura wakiwa katika eneo la mauaji katika kanisa la First  Baptist huko Sutherland Springs, Texas, Nov. 5, 2017. Mtu mmoja anayeaminika kuwa mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Marekani aitwaye Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26 ameshambulia watu kwenye kanisa moja karibu na San Anrtonio jumapili asubuhi na kuuwa watu 26 na kujeruhi wengine wasiopungua 20. Walioathirika katika shambulio hilo la kanisani kwa silaha nzito za risasi za mauaji ya halaiki ni kati ya umri wa miaka 5 hadi 72. Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na bado haijulikani sababu ya kuchukua hatua hiyo. Wachunguzi kutoka idara ya makosa ya jinai FBI na idara ya usimamizi wa vilevi, tumbaku na silaha wako Sutherland Springs Texas kiasi cha kilometa 50 kutoka San Antonio. Rais Donald Trump ameita mauaji hayo kitendo cha kikatili na kutoa wito wa maombi. Rais anafuatilia hali ilivyo akiwa Japan kituo chake cha kwanza katika ziara ya n...

Uhuru Kenyatta Atangazwa Mshindi Wa Urais Nchini Kenya Kwa Asilimia 98

Image
Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.   Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.   Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.   Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.   Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho. Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika ma...

Zambia: Kuanzia Sasa Kila Mwananchi ni Lazima Apimwe UKIMWI, Sio Hiari Tena

Image
Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba. Rais Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya serikali ya kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.

Mtoto Mchanga wa Miezi 6 Aliyejeruhiwa na Polisi Afariki Dunia

Image
Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na familia yake. Samantha Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu.

Umoja wa Mataifa Wakataa Ombi la Raila Odinga

Image
Afisa wa Umoja wa Mataifa, amekataa ombi la kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga la kutaka umoja huo kufanya tathmini mpya ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, ameunga mkono kauli ya Katibu Mkuu, Antonio Gutrres, ya kuwataka wanasiasa wa Kenya wanaopinga matokeo ya uchaguzi kufikisha masuala hayo mbele ya taasisi zenye mamlaka ya kutoa maamuzi Kikatiba.

Rais Museveni abadilisha tarehe yake wa kuzaliwa

Image
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni. Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena. Lakini nadhari nyingine imeibuka  ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70. Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena katika awamu ya sita. Museveni alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awa...

Mahakama Yatoa ONYO la Mwisho kwa Tundu Lissu

Image
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo. Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani. Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Ntobesya amedai kuwa mteja wake ana udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika. Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo  ameahirisha kesi hiyo hadi August 14/2017. Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam.

Msichana wa miaka kumi aruhusiwa kutoa mimba

Image
Msichana mjamzito. Jopo la madaktari nchini India limekubali kutoa mimba ya msichana wa umri wa miaka 10, ambaye ni muathiriwa wa ubakaji baada ya mahakama kuamuru hatua hiyo ichukuliwe. Msichana huyo anatoka mji wa Rohtak, jimbo la Haryana, kaskazini mwa nchi hiyo. Dk Ashok Chauhan ameviambia vyombo vya habari kuwa hatua hiyo sasa inaweza  kuchukuliwa wakati wowote. Mamlaka nchini India zimesema msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano  iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo, kitendo kinachoaminika kufanyika mara kadhaa. Kwa mujibu wa gazeti la India Times, polisi wamesema kuwa mtu huyo tayari amekamatwa. Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba kwa wanawake wajawazito baada ya wiki 20  bila ya idhini ya madaktari. Inahofiwa kwamba hatua kama hiyo inaweka maisha ya mwanamke hatarini. Mahakama moja nchini India iliamuru kwamba madaktari wanaweza kutoa mimba ya msichana huyo. Kupata mimba kw...

NAJUA UNAJUA ILA NAJUA HILI HUJUI ACHA NIKUJUZE WANYAMA WA AJABU DUNIANI AMBAO HUJAWAHI KUWAONA

Image

Mbunge Australia anyonyesha mtoto bungeni

Image
Senator kutoka jimbo la Queensland nchini Australia, Larissa Waters, ameweka historia bungeni hapo alipomleta kazini na kumnyonyesha mwanaye wa miezi miwili ikiwa ni mara ya kwanza na hivyo kutengeneza historia hiyo nchini humo.

Trump amwachisha kazi mkurugenzi wa FBI

Image
Aliyekuwa mkurugenzi wa FBI James Comey. Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, Marekani (FBI) ameachishwa kazi siku ya Jumanne na rais Donald Trump. Taarifa kutoka ikulu imesema Trump alichukua hatua hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa mwanasheria mkuu, Jeff Session na naibu wake, Rod Rosenstein. "Leo rais Donald Trump amemjulisha mkurugenzi wa FBI James Comey kwamba ameachishwa kazi na kuondolewa madarakani," ilisema taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na msemaji wa ikulu, Sean Spicer Jumanne jioni. Taarifa hiyo ileleza kuwa shughuli za kumtafuta mkurugenzi mpya wa idara hiyo zilikuwa zimeshaanza. Kuachishwa kazi kwa Comey kulipokelewa kwa mshangao na baadhi ya wabunge na maseneta. Wiki jana, Comey alihojiwa na kamati ya seneti kuhusu tuhuma kwamba huenda Russia iliingilia kuvuruga uchaguzi wa Marekani wa Novemba mwaka uliopita. Aidha mkurugenzi huyo wa zamani amekuwa akikabiliwa na tuhuma kwamba uamuzi wake wa k...

ushawahi kusikia kisiwa ambacho wanawake hawaruhusiwi kufika na wakifika wana.....

Image
Jopo moja la ushauri limependekeza kisiwa kimoja nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kitambuliwe kama turathi ya ulimwengu. Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kaisi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema. Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi. Jopo hilo limependekeza Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) litambue kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu. Uamuzi unatarajiwa kufanywa katika mkutano wa Unesco mwezi Julai. Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini. Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema. Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigw...

Binti wa Miaka 35 Ajitokeza Kuwania Urais Nchini Rwanda

Image
Mwanadada Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

AJALI MBAYA YA MGODI WA MAKAA YA MAWE IRAN MPAKA SASA MIILI 21 IMEOPOLEWA SHUGHULI BADO INAENDELEA

Image
Waokoaji nchini Iran wameopoa miili ya watu 21 baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe, huku zaidi ya wengine 69 wakijeruhiwa. Mlipuko huo unadhaniwa kusababishwa na kuvuja kwa gesi katika mgodi wa Zemestan-Yurt Kaskazini mwa jimbo la Golestan. Baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliokwenda katika mgodi huo kuwasaidia waliojeruhiwa. Zaidi ya wachimbaji wengine 32 wamekwama ardhini. Juhudi za uokoaji zinaendelea huku zikikwamishwa na njia nyembamba ya kuingia sambamba na uwepo wa kiwango kikubwa cha gesi ndani ya mgodi huo.

MPELELEZI AOLEWA NA GAIDI HATARI ALIEKUA ANAMCHUNGUZA

Image
Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI limethibitisha kuwa mmoja wa wafasiri wake alifunga ndoa na mwajiri wa Islamic State ambaye alikuwa akimchunguza.

RAIS JACOB ZUMA AKIONA CHA MOTO LEO SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIKUAJE? FUATANA NAMI!!

Image
Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.

Wanaharakati waandamana Washington na miji mingine 100 Marekani

Image
Maadamano ya wananchi wa Wamarekani kupinga sera za Rais   Trump kuhusu mazingira

Meli kubwa ya kijasusi ya Urusi yazama Uturuki

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** ********************* Meli ya kijasusi ya Urusi imezama baharini katika pwani ya Uturuki baada ya kugongana na meli ya kubeba mizigo, maafisa wa uchukuzi wa baharini wa Uturuki wamesema.

KIJANA KUTOKA USWAHIILINI ASIESOMA HATA DARASA 1 AUNDA NDEGE NA IMESHAFIKIA HATUA YA KURUKA!!

Image
*********************** ****** BLOG NO 1 TANZANIA !!**** ********************* Fredrick Onyango kijana wa umri wa miaka 25 huwashangaza wengi Nairobi kutokana na ndege yake ambayo licha ya kutopata masomo yoyote amefanikiwa kuiunda hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi. Onyanyo ambaye kwa miaka mingi ameishi

UTAFITI: Kuangalia TV Kupita Kiasi Hupunguza Uwezo wa Kuzalisha Mbegu za Kiume

Image
                                               BLOG NO 1 TANZANIA !!   Kuangalia TV ni sehemu ya maisha ya asilimia kubwa ya watu duniani hivi sasa, lakini utafiti umeonesha kuwa wanaume wako kwenye hatari ya kupungua uwezo wa kuzalisha mbegu za kiume pale wanapotumia muda mwingi kuangalia TV. Kabla hujaanza kubisha, soma kwa makini utafiti huu. Wenzetu husema ‘no research no right to speak’. Utafiti huo ulifanywa hivi karibuni na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen, umeonesha matokeo hayo baada ya kutumia sampuli ya vijana wa kiume 1,200. Utafiti huo uliochapishwa kwenye Jarida la Marekani la ‘Epidemiology’ ulionesha kuwa wanaume wanaopenda kuangalia TV (kwa saa tano na zaidi) walitoa wastani wa mbegu za kiume (sperm counts) milioni 37 kwa mililita moja, huku wale ambao hawakuwa na tabia ya kuangalia TV kabisa walitoa wastani wa mbegu za k...