Posts

Watu 26 wauawa kanisani Texas Marekani

Image
Askari na wafanyakazi wa dharura wakiwa katika eneo la mauaji katika kanisa la First  Baptist huko Sutherland Springs, Texas, Nov. 5, 2017. Mtu mmoja anayeaminika kuwa mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Marekani aitwaye Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26 ameshambulia watu kwenye kanisa moja karibu na San Anrtonio jumapili asubuhi na kuuwa watu 26 na kujeruhi wengine wasiopungua 20. Walioathirika katika shambulio hilo la kanisani kwa silaha nzito za risasi za mauaji ya halaiki ni kati ya umri wa miaka 5 hadi 72. Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na bado haijulikani sababu ya kuchukua hatua hiyo. Wachunguzi kutoka idara ya makosa ya jinai FBI na idara ya usimamizi wa vilevi, tumbaku na silaha wako Sutherland Springs Texas kiasi cha kilometa 50 kutoka San Antonio. Rais Donald Trump ameita mauaji hayo kitendo cha kikatili na kutoa wito wa maombi. Rais anafuatilia hali ilivyo akiwa Japan kituo chake cha kwanza katika ziara ya nchi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 4

Image

Katibu Mkuu CHADEMA Atoa Neno Uchaguzi Mdogo wa Madiwani.....Azungumzia Sakata la Wanaohamia CHADEMA

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda. Ameyasema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya ambao wameuanzisha. “Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda,”amesema Mashinji Aidha, mbali na hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka. Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhama kwa wanacha

Watetezi Haki za Wanyama Walaani Vifaranga hai Kuchomwa moto

Image
Watetezi wa haki za wanyama wamelaani kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria. Vifaranga hivyo mali ya Mary Matia (23), vyenye thamani ya Sh12.5 milioni vilikamatwa mpakani Namanga vikitokea nchini Kenya. Kuteketezwa kwa vifaranga hivyo jana Jumanne Oktoba 31,2017 kumeibua mjadala ikielezwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria. Kazi ya kuviteketeza eneo la Namanga wilayani Longido ilifanyika ikishuhudiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Mifugo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Akizungumza wakati wa kuviteketeza vifaranga hivyo, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasebwa amesema kazi hiyo imefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya mwaka 2003. Pia, amesema Serikali mwaka 2007 ilitoa tangazo kupiga marufuku kuingizwa nchini vifaranga vya kuku na mayai. Hata hivyo, watu mbalimbali wamehoji ulazima wa kuvitekete

Basi Lagonga Treni na Kujeruhi watu Wawili

Image
Watu wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la Nkondo lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza baada ya kugonga kichwa cha treni eneo la Karogho Relini katika Manispaa ya Shinyanga. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa tatu usiku juzi barabara kuu iendayo Maganzo wakati basi hilo lenye namba za usajiri T 693 BUW aina ya Youtong mali ya Kampuni ya Nkondo likiendeshwa na dereva Emmanuel Warengo (34). Kamanda alisema katika ajali hiyo, watu wawili Ramadhani Juma (38) na Eva Brown (29) walijeruhiwa kwa kuumia kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kupata matibabu.  Alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutochukua tahadhari wakati wa kuvuka barabara katika njia ya treni na alikimbia baada ya ajali hiyo na Polisi wanaendelea kumtafuta. Katika matukio mengine, Polisi imefanya oparesheni na kuwakamata watuhumiwa 29 wa makosa mbalimbali, kati ya hao saba kwa tukio la u

MIMI SIO MBUNGE WA NDIYO MZEE HATA RAIS ANALIELEWA HILO- BASHE

Image
Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee. Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.   "Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko'  "Huo ndio msimamo wangu na siku naomba kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali" alisema Bashe Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamsha

MAGAZETI YA TANZANIA NA MAGAZETI YA ULAYA & MICHEZO LEO 3 NOVEMBER 2017

Image