Msichana wa miaka kumi aruhusiwa kutoa mimba

Msichana mjamzito.
Jopo la madaktari nchini India limekubali kutoa mimba ya msichana wa umri wa miaka 10,
ambaye ni muathiriwa wa ubakaji baada ya mahakama kuamuru hatua hiyo ichukuliwe.
ambaye ni muathiriwa wa ubakaji baada ya mahakama kuamuru hatua hiyo ichukuliwe.
Msichana huyo anatoka mji wa Rohtak, jimbo la Haryana, kaskazini mwa nchi hiyo.
Dk Ashok Chauhan ameviambia vyombo vya habari kuwa hatua hiyo sasa inaweza
kuchukuliwa wakati wowote.
kuchukuliwa wakati wowote.
Mamlaka nchini India zimesema msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano
iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo, kitendo kinachoaminika kufanyika mara kadhaa.
iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo, kitendo kinachoaminika kufanyika mara kadhaa.
Kwa mujibu wa gazeti la India Times, polisi wamesema kuwa mtu huyo tayari amekamatwa.
Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba kwa wanawake wajawazito baada ya wiki 20
bila ya idhini ya madaktari.
bila ya idhini ya madaktari.
Inahofiwa kwamba hatua kama hiyo inaweka maisha ya mwanamke hatarini.
Mahakama moja nchini India iliamuru kwamba madaktari wanaweza kutoa mimba ya msichana huyo.
Kupata mimba kwa msichana huyo kumezua hisia mbali mbali hususan kwenye mitandao ya kijamii,
huku baadhi ya watu wakitaka babake wa kambo anyetuhumiwa kumbaka achukuliwe
hatua kali za kisheria.
huku baadhi ya watu wakitaka babake wa kambo anyetuhumiwa kumbaka achukuliwe
hatua kali za kisheria.
Comments
Post a Comment