KABURU ATHIBITISHA MO, POPPE HAWANA KINYONGO TENA... asema sasa ni "Nguvu Moja" kuziua Mwadui FC na Mbao


KAULI mbiu ya klabu ya Simba ni maeneo mawili mazito lakini yanayoonekana ni yenye maana kubwa katika maisha ya watu wanaotamani kupata mafanikio, “Nguvu Moja.” Maneno haya yametumika katika vikao viwili tofauti ndani ya siku tatu, kikao kimoja kikiwa ni cha wajumbe wa Kamati ya Utendaji dhidi wa wajumbe wenzao, kapteni Zakaria Hans Poppe ambaye alikuwa ametangaza kujiuzulu nafsi zake zote katika klabu hiyo. Kamanda huyo wa zamani wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alikuwa amekerwa na kitendo cha viongozi wenzake katika Simba kuingia mkataba wenye thamani ya sh bil 4.9 na kampuni ya Sportpesa ya Kenya. Inadaiwa kuwa Hans Poppe alikuwa akipinga Simba kuingia mkataba huo bila kuujadili kwa kina, lakini pia bila kumshirikisha mwanachama mwenzao anayeisaidia Simba kwa hali na mali, “Mohammed Dewji” “MO”. Lakini kikao cha siku moja baina ya viongozi na Poppe kikamaliza udhia na mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili akatengua uamuzi wake na kurejea kazini. Baada ya kikao hicho wajumbe wote wa kamati ya utendaji wakiongozwa na rais wa Simba, Evans Aveva wakafanya kikao kingine na Mohammed Dewji ambaye naye alikuwa ametangaza mapema kwamba hakufurahishwa na mkataba wa Sortpesa. Taarifa ambayo imetolewa juzi na makamu wa rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange "Kaburu” imesema kwamba kikao hicho na MO kilikuwa na mafanikio makubwa na wote kwa pamoja wameendelea kufuta tofauti zao na kuongeza nguvu ya kusaidia Simba hadi mwisho. “Tumefanya kikao na MO hakikuwa kirefu sana lakini kilikuwa kizito. Tunashukuru kwamba ameelewa dhamira yetu naye amekubali kwamba nia yetu ilikuwa njema kuisaidia Simba. Mambo yote yamekwisha na tuanaendelea na jukumu letu la kuifanya Simba kuwa klabu ya kisasa zaidi,” amesema kaburu. Kaburu amesema kwamba kwa sasa hakuna kiongozi yeyote katika Simba mwenye kinyongo akiwemo MO mwenyewe, na kwamba wote wameamua kuunganisha nguvu zao kuhakikisha kwamba Simba inamaliza mechi zake mbili zilizobaki ikiwemo ile ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC na mwadui katika mechi ya Ligi Kuu kwa ushindi. “Wote tumemaliza kila kitu na kila mmoja akili yake ni kuangalia mechi zetu ile ya Jumamosi dhidi ya Mwadui na ile ya tarehe 27 dhidi ya Mbao ambayo imeweza kutupa uwakika wa kushiriki michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU

Hii hapa ratiba ya michuano yote mikubwa ya leo hii,Shirikisho,Epl,La Liga,Bundesliga na Seria A