MSUVA: NITAHAKIKISHA YANGA INATETEA UBINGWA WA LIGI KUU BARA KWANZA



KINARA wa ufungaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amesema kuwa kipaumbele kikubwa kwake ni kuhakikisha Yanga inatetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na sio kuwaza mafanikio binafsi. Msuva ambaye ni kinara wa ufungaji katika klabu yake ya Yanga ambapo kabla ya mchezo na Prison alikuwa na mabao 12
katika orodha ya wafungaji, amekuwa nyota muhimu zaidi msimu huu. “Ni kweli nipo kwenye nafasi nzuri ya kubeba tuzo ya ufungaji lakini hicho sio kipaumbele changu wakati huu, nawaza kuisaidia timu kwanza itetee taji la Ligi Kuu bara,” alisema Msuva. “Tupo kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwasababu mechi zetu nyingi tutacheza Dar es Salaam ambako kuna uwanja mzuri zaidi,” aliongeza winga huyo mwenye kasi. Yanga inakabiriwa na mchezo mmoja tu ugenini dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU

Hii hapa ratiba ya michuano yote mikubwa ya leo hii,Shirikisho,Epl,La Liga,Bundesliga na Seria A