Posts

Showing posts from October, 2017

HEBU SIKILIZA MANENO YA MAKONDA HAPA!! KUHUSU NYALANDU NA ZITTO KABWE ALAFU NIANDIKIE MAONI YAKO HAPO KWENYE COMMENT

Image

UPDATES: Zitto Aachiwa kwa Dhamana, Aisubiri Serikali Mahakamani

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani. Kwa upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo. "Tunasubiri ni lini watatupel...

Wizara Ya Afya Yatoa Tahadhari Ya Ugonjwa Wa Hatari wa Marburg

Image
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba, 2017. Maeneo yaliyoathirika  na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya Mashariki ya nchi, ambayo  inapakana n nchi ya  Kenya. Hadi kufikia  tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao   wamepoteza maisha. Wizara  inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi  katika mikoa yote ya Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi  katika mikoa ambayo inapakana na na nchi  ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera). Ugonjwa wa Marburg  unafanana sana na ugonjwa wa Ebola. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama  “Marburg Virus”, navyo vipo katika jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus). Ugonjwa huu ni miong...

Uhuru Kenyatta Atangazwa Mshindi Wa Urais Nchini Kenya Kwa Asilimia 98

Image
Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.   Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.   Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.   Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.   Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho. Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika ma...

LOWASA AMKARIBISHA NYALANDU KWA KUSEMA "TUMELAMBA DUME"

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM. Akionyesha kuwa na furaha leo Jumatatu wakati akiongea, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”. Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango. Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani. “Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne. “Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowa...

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma baada ya Rais Magufuli "Kumtumbua"

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wa zamani, Jordan Rugimbana amesema hakuna kilichobadilika kwake kwa sababu mtumishi wa umma ni kama askari ambaye hachagui uwanja wa kupigana vita. Rugimbana aliyeachwa katika mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 30, 2017 alipokabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Dk Binilith Mahenge. Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Rugimbana amesema, "Mtumishi wa umma ni kama askari, hachagii uwanja wa kupigana vita, kwa lugha nyingine hakuna kilichobadilika nipeni muda mtaelewa." Amesema anakwenda uraiani lakini jukumu lake sasa litakuwa ni kulipa fadhila kwa Rais Magufuli kwa kumchagua kuwa miongoni mwa wasaidizi wake wa kwanza katika Serikali aliyoiunda mwaka 2015. Rugimbana amesema anachomuahidi Rais ni kuwa atakuwa raia mtiifu, mwaminifu na ataendelea kuwa timu Magufuli. Amewasifu wakuu wa wilaya akisema ni watiifu, wamekuwa wakiuliza na kupokea ushauri wanaopewa. K...

Kauli ya Wema Sepetu Kuhusu Hali ya Tundu Lissu na Nyalandu Kuihama CCM

Image
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa anajisikia furaha na amani kuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa anaendelea vyema kadili siku zinavyokwenda lakini pia amegusia sakata la Nyalandu kujitoa CCM. Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa anakula chakula akiwa hospitali Nairobi na kusema anajisikia vizuri kuona shujaa wao anaendelea vizuri. "Ni jambo jema kumuona shujaa wetu anaendelea vyema kweli Mungu ni mwema siku zote, lakini pia nikiwa mkubwa nitahitaji kuwa kama Lazaro Nyalandu" aliandika Wema Sepetu Wema Sepetu ameweka ujumbe huu masaa kadhaa toka Lazaro Nyalandu alipotangaza kujivua uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuandika barua kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Zitto Kabwe ampongeza Nyalandu

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amempa tano Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi. Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge. Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu, umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Kila la kheri." Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali. 

Irene Uwoya Afunguka Baada ya Kufunga Ndoa na Dogo Janja

Image
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake. Irene Uwoya kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha hilo na kusema kuwa anampenda sana msanii huyo na kudai huyo ndiye mwanaume wa ndoto yake hivyo anafurahi kuona wamefunga pingu ya maisha.  "Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha. Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe" aliandika Irene Uwoya. Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.

Breaking News: Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge Singida Kaskazini

Image
  NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa. AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutoridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA. VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mp...