Posts

Watu 26 wauawa kanisani Texas Marekani

Image
Askari na wafanyakazi wa dharura wakiwa katika eneo la mauaji katika kanisa la First  Baptist huko Sutherland Springs, Texas, Nov. 5, 2017. Mtu mmoja anayeaminika kuwa mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Marekani aitwaye Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26 ameshambulia watu kwenye kanisa moja karibu na San Anrtonio jumapili asubuhi na kuuwa watu 26 na kujeruhi wengine wasiopungua 20. Walioathirika katika shambulio hilo la kanisani kwa silaha nzito za risasi za mauaji ya halaiki ni kati ya umri wa miaka 5 hadi 72. Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na bado haijulikani sababu ya kuchukua hatua hiyo. Wachunguzi kutoka idara ya makosa ya jinai FBI na idara ya usimamizi wa vilevi, tumbaku na silaha wako Sutherland Springs Texas kiasi cha kilometa 50 kutoka San Antonio. Rais Donald Trump ameita mauaji hayo kitendo cha kikatili na kutoa wito wa maombi. Rais anafuatilia hali ilivyo akiwa Japan kituo chake cha kwanza katika ziara ya n...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 4

Image

Katibu Mkuu CHADEMA Atoa Neno Uchaguzi Mdogo wa Madiwani.....Azungumzia Sakata la Wanaohamia CHADEMA

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda. Ameyasema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya ambao wameuanzisha. “Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda,”amesema Mashinji Aidha, mbali na hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka. Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhama kwa wanacha...

Watetezi Haki za Wanyama Walaani Vifaranga hai Kuchomwa moto

Image
Watetezi wa haki za wanyama wamelaani kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria. Vifaranga hivyo mali ya Mary Matia (23), vyenye thamani ya Sh12.5 milioni vilikamatwa mpakani Namanga vikitokea nchini Kenya. Kuteketezwa kwa vifaranga hivyo jana Jumanne Oktoba 31,2017 kumeibua mjadala ikielezwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria. Kazi ya kuviteketeza eneo la Namanga wilayani Longido ilifanyika ikishuhudiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Mifugo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Akizungumza wakati wa kuviteketeza vifaranga hivyo, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasebwa amesema kazi hiyo imefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya mwaka 2003. Pia, amesema Serikali mwaka 2007 ilitoa tangazo kupiga marufuku kuingizwa nchini vifaranga vya kuku na mayai. Hata hivyo, watu mbalimbali wamehoji ulazima wa kuvitekete...

Basi Lagonga Treni na Kujeruhi watu Wawili

Image
Watu wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la Nkondo lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza baada ya kugonga kichwa cha treni eneo la Karogho Relini katika Manispaa ya Shinyanga. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa tatu usiku juzi barabara kuu iendayo Maganzo wakati basi hilo lenye namba za usajiri T 693 BUW aina ya Youtong mali ya Kampuni ya Nkondo likiendeshwa na dereva Emmanuel Warengo (34). Kamanda alisema katika ajali hiyo, watu wawili Ramadhani Juma (38) na Eva Brown (29) walijeruhiwa kwa kuumia kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kupata matibabu.  Alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutochukua tahadhari wakati wa kuvuka barabara katika njia ya treni na alikimbia baada ya ajali hiyo na Polisi wanaendelea kumtafuta. Katika matukio mengine, Polisi imefanya oparesheni na kuwakamata watuhumiwa 29 wa makosa mbalimbali, kati ya hao saba kwa tukio ...

MIMI SIO MBUNGE WA NDIYO MZEE HATA RAIS ANALIELEWA HILO- BASHE

Image
Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee. Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.   "Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko'  "Huo ndio msimamo wangu na siku naomba kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali" alisema Bashe Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamsha...

MAGAZETI YA TANZANIA NA MAGAZETI YA ULAYA & MICHEZO LEO 3 NOVEMBER 2017

Image

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Novemba 1

Image

HEBU SIKILIZA MANENO YA MAKONDA HAPA!! KUHUSU NYALANDU NA ZITTO KABWE ALAFU NIANDIKIE MAONI YAKO HAPO KWENYE COMMENT

Image

UPDATES: Zitto Aachiwa kwa Dhamana, Aisubiri Serikali Mahakamani

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani. Kwa upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo. "Tunasubiri ni lini watatupel...

Wizara Ya Afya Yatoa Tahadhari Ya Ugonjwa Wa Hatari wa Marburg

Image
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba, 2017. Maeneo yaliyoathirika  na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya Mashariki ya nchi, ambayo  inapakana n nchi ya  Kenya. Hadi kufikia  tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao   wamepoteza maisha. Wizara  inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi  katika mikoa yote ya Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi  katika mikoa ambayo inapakana na na nchi  ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera). Ugonjwa wa Marburg  unafanana sana na ugonjwa wa Ebola. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama  “Marburg Virus”, navyo vipo katika jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus). Ugonjwa huu ni miong...

Uhuru Kenyatta Atangazwa Mshindi Wa Urais Nchini Kenya Kwa Asilimia 98

Image
Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.   Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.   Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.   Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.   Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho. Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika ma...

LOWASA AMKARIBISHA NYALANDU KWA KUSEMA "TUMELAMBA DUME"

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM. Akionyesha kuwa na furaha leo Jumatatu wakati akiongea, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”. Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango. Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani. “Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne. “Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowa...