Asasi 30 Afrika zalaani uvamizi Clouds
BLOG NO 1 TANZANIA !! Dar es Salaam. Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani. Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Asasi hizo zinazohusika na utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa habari zilikutana hivi karibuni mjini Kampala nchini Uganda katika mkutano uliokuwa ukizungumzia uhuru wa kujieleza na kupata habari. Tanzania kwenye mkutano huo iliwakilishwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) , miongoni mwa mijadala iliyotawala ni kukemea vitisho na vitendo vya kunyanyasa waand...