Baba wa Miaka 60 Akamatwa akipata Penzi la Mwanaye wa Kumzaa

MKAZI wa Kata ya Wailes, Manispaa ya Lindi, Issa Nambaluka (60), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14. 

Nambaluka alifikishwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Erasto Phili na kusomewa mashtaka na Mwanasheria wa Serikali, Emmanuel John.

John alidai kwamba kati ya Novemba na Desemba, mwaka jana, majira ya usiku,mshitakiwa kwa makusudi huku akijua anachokifanya ni kosa, alimbaka mlalamikaji ambaye ni mtoto wake wa kumzaa, ambaye ni mwanafuzi wa darasa la sita.

Mwanasheria huyo alidai kutokana na kitendo hicho, mshitakiwa amefanya kosa kwa mujibu wa vifungu vya Sheria 158 (1) na 130 (2) (e) na 131 (i) ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2002.

Pia aliiambia Mahakama hiyo kwamba mshitakiwa alikuwa akimfanyia kitendo hicho, kipindi ambacho mkewe akiwa ametoka kwenda kijijini kwao, Litehu wilayani Lindi kusalimia wazazi wake.

Mshitakiwa alikana makosa aliyoshitakiwa nayo na kupelekwa mahabusu, baada ya upande wa Jamhuri kuomba kuzuia dhamana, kwa kile kilichodaiwa ni kulinda usalama wake, kutokana na jamii kuchukizwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na mshitakiwa.

Shauri hilo limepangwa kutajwa tena katika mahakama hiyo wiki mbili zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU