BREAKING NEWS!! MASOGANGE AKAMATWA NA KULAZWA NDANI KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA!!


Taarifa zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na ishu ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange na kinachoendelea, zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu na pia kufuatilia Global TV Online.

Source: Global Publisher

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU