Kim Jong Un alitoa amri ya kuuawa kwa kaka yake
BLOG NO 1 TANZANIA !!

WIZARA mbili za Korea Kaskazini zilipanga mauaji ya Kim Jong Nam kutokana na amri ya kaka yake wa kambo, kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, shirika la kijasusi la Korea Kusini limesema.
WIZARA mbili za Korea Kaskazini zilipanga mauaji ya Kim Jong Nam kutokana na amri ya kaka yake wa kambo, kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, shirika la kijasusi la Korea Kusini limesema.
Wabunge huko Seoul, ambao walipewa taarifa ya maafisa wa kijasusi wa nchi hiyo, walisema Wizara za Mambo ya Nje na ile ya Usalama wa taifa za Korea Kaskazini ziliwapa kazi washukiwa wawili wa kike katika mauaji ya Kim.
“Mauaji ya Kim Jong Nam ni tendo la kigaidi lililoamriwa na Kim Jong Un,” mbunge wa Korea Kusini Kim Nyung-kee alisema kupitia televisheni. Operesheni ilifanywa na makundi mawili ya mauaji na moja likiwa linatoa msaada.”
Korea Kaskazini imekuwa ikikana kuhusika na mauaji ya Kim Jong Nam na imekuwa ikivishutumu vyombo vya habari vya Korea Kusini kwa kuandika “habari za uongo.”
Kim Jong Nam alisogelewa na wanawake wawili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur siku ya Februari 13, akiwa njiani kuelekea Macau ambayo ni sehemu ya China.
Alifariki akiwa njiani kwenda hospitali, chini ya dakika 20 baadae, kulingana na wapelelezi wa Malaysia, ambao walisema wanawake walimshambulia kwa kutumia sumu inayoshambulia mfumo wa fahamu ya VX nerve agent.
Watuhumiwa watatu hadi sasa wamewekwa kuzuizini, wakiwemo wawili kutoka nchini Vietnam na mmoja kutoka Indonesia ambaye alionekana kwenye picha za video 'akipaka' kitu kwenye uso wa Kim.
Makundi ya mauaji yalifanya kazi tofauti
Katika mkutano na waandishi wa habari, mbunge Kim alisema kwamba makundi mawili ya wauaji yalikuwa yakifanya kazi tofauti kabla ya kukutana huko Malaysia muda mfupi kabla ya mauaji.
Alisema kundi la kwanza, lilikuwa na jasusi kutoka Korea Kaskazini Ri Jae Nam na mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje Ri Ji Hyong, na lilimpa kazi mtuhumiwa wa Vietnam, Doan Thi Huong.
Wakati huo huo, kundi la pili, pia lilimhusisha jasusi kutoka Korea Kaskazini, O Jong Gil, na mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Hong Song Hac, na lilimwajiri mtuhumiwa kutoka Indonesia Siti Aisyah.
Kim alisema watu wote wanne wa makundi hayo ya mauaji walikimbilia Korea Kaskazini baada ya mauaji hayo.
Kundi kubwa zaidi ambalo lilikuwa likitoa msaada kwa makundi mawili ya awali, yaliwahusisha wafanyakazi wa ubalozi wa Korea Kaskazini, na pia wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Korea Kaskazini la Koryo na pia shirika binafsi la biashara.
Kim hata hivyo hakusema ni kwa namba gani raia mwingine wa Korea Kaskazini ambaye tayari yupo kizuizini Ji Jong Chol, mwenye umri wa miaka 46, alivyohusika.
Kufa baada ya dakika 20
Taarifa za maabara kutoka kwa mwili wa Kim zilionyesha kuwa alifariki ndani ya dakika 15 hadi 20 baada ya shambulizi, Waziri wa Afya wa Malaysia Dokta Subramaniam Sathasivan alisema Jumapili.
Aliongeza kifo cha Kim kilikuwa “cha maumivu makali.”
Mamlaka nchini Malaysia bado zimeushikilia mwili wa Kim na zimesema hazitautoa mpaka pale watapokea taarifa za kinasaba kutoka kwa ndugu wa karibu pamoja na alama za mwilini ili kumtambua Kim.
Mwandishi Yoonjung Seo alichangia katika taarifa hii..
Comments
Post a Comment