LEICESTER CITY YAIPASUA LIVERPOOL 3G YAIKANDAMIZA TAIRI ZA BAJAJI 3-1
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Leicester City wamejikokota na kupanda hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuizaba Liverpool kwa mabao 3-1.
Leicester walionesha kiwango cha juu,na magoli mawili kutoka kwa JamieVardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater yaliididimiza Liverpool.
Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig Shakespeare, aliyechukua mikoba ya Ranieri, mabingwa hao wa England walicheza kama mabingwa watetezi.
Goli la kwanza la Jamie Vadry limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi murua kutoka kwa Marc Albrighton iliyomfikia Vardy.
Magoli haya ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017.
Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote.
BLOG NO 1 TANZANIA !! Pamoja na kwamba awali, beki wa kati wa Simba Mwanjale alionekana anarejea na kuwa fiti, daktari amemuongezea siku zaidi. Mwanjale atakuwa nje kwa matibabu kwa siku 15 kabla ya kurejea mazoezini. Imeelezwa, goti aliloumia linahitaji mapumziko wakati akiendelea na matibabu. Matarajio ni kuanza mazoezi wiki ijayo ingawa inawezekana hatacheza mechi mbili za mwanzo au zote za Kanda ya Ziwa.
Jaji Mohamed Chande Othman akimpa mkono wa pole Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Upendo H. Msuya apokuwa amefiwa na mwanaye aliyekuwa nchini Malaysia. (picha na Mary Gwera, MAHAKAMA YA TANZANIA
Comments
Post a Comment