MAKONDA ALALAMIKA KUTUPIWA JINI NA WATU 12 ALIOWATAMBUA!! SOMA HABARI HIO HAPA!!
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Katika mapambano yanayoendelea ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya pamoja na watumiaji, kuna watu 12 waliokuwa wamepanga njama za kunitupia majini lakini hawakufanikiwa kutokana na kinga ya maombi kutoka kwa viongozi wa dini.
Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda alipokuwa katika semina ya Masheikh, wanazuoni, maimamu na walimu wa Quran Tanzania kupitia jumuiya ya walimu wanaosomesha Quran Tanzania (JAWAQUTA).
Makonda alisema waumini hao 12 waliandaa mbuzi mweupe ili kumtoa kafara na yeye alifanikiwa kuwatambua kupitia mtandao wake.
Aidha alisema, haamini kama waumini hao ni wa dini ya kiislamu, bali ni kundi la watu waliokuwa wamevalia kanzu kwa utambulisho huo na kwamba huenda walitumika kuwalia watu fedha zao.
Pia aliwaomba viongozi hao kuendelea kutoa ushirikiano katika vita aliyoianzisha ya dawa za kulevya.

Comments
Post a Comment