MANCHESTER UNITED NA GUNDU LA STAMFORD BRIDGE JE WATAVUNJA MWIKO?
MANCHESTER, ENGLAND. HABARI mbaya Manchester United. Mechi ijayo ya Kombe la FA wamepangiwa kucheza kwenye uwanja ambao hawajawahi kushinda taji Oktoba 2012.
Baada ya kuwachapa Blackburn Rovers 2-1, Man United wanaonolewa na Jose Mourinho wamepangiwa kucheza na Chelsea katika mechi ya hatua ya robo fainali ya Kombe la FA ambapo mechi hiyo itapigwa Stamford Bridge.
Mourinho atarejea tena kwenye uwanja huo uliokuwa wa timu yake ya zamani akiwa na kumbukumbu ya kuchapwa 4-0 mara ya mwisho alipokwenda hapo na kikosi chake cha Man United, lakini kitu kingine ni gundu la wababe hao wa Old Trafford kwamba hajawahi kushinda mara zote walizokwenda huko London Magharibi tangu 2012.
Katika droo hiyo ya ratiba iliyopangwa Jumapili usiku, ukiweka kando kipute cha Chelsea na Man United, mechi nyingine za robo fainali, Tottenham Hotspur watakipiga na Millwall, wakati Middlesbrough atacheza na mshindi kati ya mechi ya Huddersfield na Manchester City ambao itabidi walirudiane baada ya sare ya bila kufungana katika mechi yao ya kwanza.
Arsenal wamepata mchekea wa kucheza na timu ya mchangani, Lincoln City baada ya kuwafunga Sutton United 2-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku
Comments
Post a Comment