BLOG NO 1 TANZANIA !! Pamoja na kwamba awali, beki wa kati wa Simba Mwanjale alionekana anarejea na kuwa fiti, daktari amemuongezea siku zaidi. Mwanjale atakuwa nje kwa matibabu kwa siku 15 kabla ya kurejea mazoezini. Imeelezwa, goti aliloumia linahitaji mapumziko wakati akiendelea na matibabu. Matarajio ni kuanza mazoezi wiki ijayo ingawa inawezekana hatacheza mechi mbili za mwanzo au zote za Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wa zamani, Jordan Rugimbana amesema hakuna kilichobadilika kwake kwa sababu mtumishi wa umma ni kama askari ambaye hachagui uwanja wa kupigana vita. Rugimbana aliyeachwa katika mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 30, 2017 alipokabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Dk Binilith Mahenge. Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Rugimbana amesema, "Mtumishi wa umma ni kama askari, hachagii uwanja wa kupigana vita, kwa lugha nyingine hakuna kilichobadilika nipeni muda mtaelewa." Amesema anakwenda uraiani lakini jukumu lake sasa litakuwa ni kulipa fadhila kwa Rais Magufuli kwa kumchagua kuwa miongoni mwa wasaidizi wake wa kwanza katika Serikali aliyoiunda mwaka 2015. Rugimbana amesema anachomuahidi Rais ni kuwa atakuwa raia mtiifu, mwaminifu na ataendelea kuwa timu Magufuli. Amewasifu wakuu wa wilaya akisema ni watiifu, wamekuwa wakiuliza na kupokea ushauri wanaopewa. K...
Comments
Post a Comment