Waziri Mkuu wa zamani ahoji, Trump anavuta nini maaana haelewi Akili zake?
STOCKHOLM, SWEDEN
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Sweden, Carl Bildt, amemjia juu Rais wa Marekani, Donald Trump, akihoji kiongozi huyo wa juu kabisa katika taifa hilo kubwa duniani amewahi kuwa mvutaji wa ‘kilevi’ cha aina gani.
Bildt amefanya shambulizi hilo dhidi ya Trump kupitia akaunti yake ya twitter, na ingawa hakubainisha moja kwa moja lakini huenda anahoji kama Trump amewahi kuvuta bangi au dawa nyingine za kulevya na msingi wake wa kuhoji ni kutokana na baadhi ya matendo yanayodaiwa kutolingana na hadhi ya rais anayoyafanya Trump katika Ikulu ya Marekani – White House.
Pamoja na kuwa waziri mkuu, Carl Bildt ambaye pia amepata kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden alikerwa na kitendo cha Trump kuitaja Sweden katika kutetea uamuzi wake wa kupiga marufuku raia wa baadhi ya nchi kuingia Marekani.
Katika kutetea uamuzi wake, Trump alitumia taarifa za kuwapo kwa tishio la shambulizi la ugaidi nchini Sweden, shambulizi ambalo hata hivyo, halikutokea.
“Tazama nchi kama Sweden na Ujerumani zinavyokabiliwa na matukio ya kigaidi,” alisema Trump, kauli ambayo imemkera Bildt kiasi cha kufikia uamuzi huo wa kuhoji kama kiongozi huyo mpya wa Marekani amewahi “kuvuta” ama la?
Bildt aliandika katika akaunti yake ya twitter; “Sweden? Shambulio la kigaidi? Hivi huyu amekuwa akivuta nini?” akaongeza; “Kuna maswali mengi ya kujiuliza.”
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara mjini Melbourne, Florida, Jumamosi iliyopita, Trump alizitaja nchi za Ulaya akitolea mfano wa Sweden na Ujerumani kuwa ni sehemu ya sababu zilizochangia Marekani kuweka masharti magumu kwa wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati kuingia nchini kwake.
“Ni lazima tuhakikishe nchi yetu inabaki salama. Ukitazama kile kinachoendelea nchini Ujerumani, ukitazama kile kilichotokea usiku uliopita kule Sweden,” Trump aliwaeleza watu waliokuwa wakimsikiliza, akaendelea; “Sweden, nani anayeweza kuamini hili? Sweden. Wamewachukua wengi (wahamiaji). Kwa sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa kuliko walivyodhani. Ukitazama kile kinachotokea Brussels. Ukitazama kile kinachotokea maeneo mbalimbali duniani. Tazama kwa umakini. Tazama kule Paris.”
Licha ya ujanja huo wa Trump, hakuna tukio lolote la kigaidi lenye kuhusiana na wakimbizi kutoka nchi za Mashariki ya Kati ndani ya Sweden kwa siku za karibuni.
“Trump ametoa mfano wa shambulizi la kigaidi ambalo halipo na halikuwahi kutokea,” gazeti la Guardian liliandika. “Donald Trump inaonekana ndiye amefanya shambulizi la kigaidi dhidi ya Sweden,” liliandika gazeti la Huffington Post.
“Donald Trump anaonekana amepandikiza shambulizi la kigaidi Sweden wakati wa hotuba yake huko Florida,” liliandika gazeti la Independent la Uingereza, wakati Shirika la Habari la Reuters nalo likiandika; “Trump ni kama amefanya shambulizi la kigaidi Sweden.”
Jarida la Liberal nalo limemtuhumu Trump kwamba ‘ametengeneza’ shambulizi la kigaidi kwa kuwa inawezekana hivi karibuni alitazama kipindi cha televisheni cha Tucker Carlson.
Bildt amepata kuwa waziri mkuu wa Sweden kuanzia mwaka 1991 hadi 1994, na baadaye kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake kuanzia mwaka

Comments
Post a Comment