ARSENAL YAGONGWA TENA 5G HII AIBU YA MWAKA WATOLEWA UEFA KWA 10-2
BLOG NO 1 TANZANIA !!

Baada ya kufungwa 5-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bayern Munich, Arsenal imekubali kichapo kingine kikubwa cha 5-1 kutoka kwa miamba hiyo ya Ujerumani. Kwa matokeo hayo, Arsenal imeaga Champions League kwa jumla ya magoli 10-2. Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 20 kupitia kwa Theo Walcott na kudumu hadi mapumziko. Dakika ya 53 sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny akalambwa kadi nyekundu iliyofuatiwa na penalti iliyozaa goli la kusawazisha mfungaji akiwa Robert Lewandowski. Bayern ikafunga tena kupitia kwa Arjen Robben dakika ya 68, Douglas Costa dakika ya 78 huku Arturo Vidal akahitimisha karamu ya magoli kwa kutupia wavuni michomo miwili dakika ya 80 na 85

Comments
Post a Comment