Barcelona yalambwa 2-1 Hispania,hesabu za ubingwa shakani.

                                                    BLOG NO 1 TANZANIA !!


BARCELONA imetibua hesabu zake za ubingwa wa La Liga hii ni baada ya usiku huu kufungwa mabao 2-1 na Deportivo La Coruna huko Estadio Municipal de Riazor.

Katika mchezo huo ilishuhudiwa kocha wa Barcelona,Luis Enrique,akikifanyia mabadiliko matano kikosi chake kutoka katika kikosi kilichoifunga Psg mabao 6-1 kwenye ligi ya mabingwa Ulaya huku Neymar akiwa nje kwa majeruhi,iliwachukua wenyeji Deportivo La Coruna dakika 40 tu kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Joselu.

Bao la pili la Deportivo La Coruna limefungwa na Alex Bergantiños García kwa kichwa katika dakika ya 74 akiunganisha mpira wa kona.Bao la Barcelona limefungwa na Luis Suarez katika dakika ya 46.

Kichapo hicho kimeiacha Barcelona katika nafasi ya kwanza na pointi zake 60,pointi moja mbele ya Real Madrid yenye pointi 59 huku pia ikiwa na michezo miwili mkononi.Deportivo imefikisha pointi 27 na kupanda mpaka nafasi ya 15.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU