BASATA yaufungia wimbo wa Nay wa Mitego “WAPO”

                                            BLOG NO 1 TANZANIA !!


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo Wapo ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitego kutumika kwa namna yoyoye ile.
Hali kadhalika limeonya watu wote wanaotumia kazi za wasanii zilizopigwa marufuku na baraza hilo kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria za nchi na kwamba watakaobainika kuzitumia watachukuliwa hatua kali.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amewataka wasanii na wadau wa kazi za sanaa nchini kuzingatia maadili na ubunifu wa hali ya juu katika kufanya kazi za sanaa.
“Baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yanayofanyika hayaachi taifa na wasanii katika hali zisizo salama, baraza litahakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi zozote za sanaa,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU