Breaking News: Tundu Lissu Achaguliwa Kuwa Rais wa TLS Kwa Ushindi wa Asilimia 88
BLOG NO 1 TANZANIA !!

Mawakili wakiendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society.

Mgombea Uraisi wa Tanganyika Law Society (TLS )Mhe Tundu Antiphas Lissu akipiga kura akiwa na mke wake Wakili Alicia Lissu

.

Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.
Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama wa TLS wamekutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.
Matokeo ni kama ifuatavyo:
Urais: Kura zilizopigwa 1682
- Tundu Lissu 1411 sawa na asilimia 88
- Francis Stolla 64
- Victoria Mandari 176
- Godwin Mwapongo 64
==>Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.
Council Members
- Jeremiah Motebesya
- Gida Lambaji
- Hussein Mtembwa
- Aisha Sinda
- Steven Axweso
- David Shilatu
- Daniel Bushele
Mawakili wakiendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society.
Mgombea Uraisi wa Tanganyika Law Society (TLS )Mhe Tundu Antiphas Lissu akipiga kura akiwa na mke wake Wakili Alicia Lissu
Comments
Post a Comment