CHARLES HILLARY AWATAKA WATANZANIA KUICHANGIA SERENGETI BOYS HUKU AKITHIBITISHA KUKAMILIKA KWA KORABO YA DIAMOND NA ALIKIBA...
BLOG NO 1 TANZANIA !!

Kamati ya kuhamasisha ushiriki wa Serengeti Boys katika fainali za vijana chini ya miaka 17 Afrika, imewaomba Watanzania kutoa michango yao ili kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa 17 Serengeti Boys inayotarajia kwenda nchini Gabon mwezi Mei kushiriki fainali za AFCON.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya Serengeti boys Charles Hillary wakati wa mkutano na waadishi wa habari uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumzia mikakati ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo.
Hillary amewaomba wapenda soka na Watanzania wote kwa ujumla, kutoa michango yao ya hali na mali ili kuisaidia timu hiyo kwani lengo lao kuu ni kuhakikisha timu hiyo inakwenda India kushiriki fainali za kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.
Pia ameyataka mashirika makubwa na wao kutoa mchango wao ili kuweza kufikia malengo.
Kwa Upande wake mjumbe wa kamati hiyo Maulid Kitenge amesema tayari ala za wimbo wa kuhamasisha uchangiaji umeshakamilika na kinachosubiriwa ni wasanii Diamond na Ali Kiba kuingiza sauti ili wimbo huo ukamilike na kuanza kutumika katika kampeni za uhamasishaji wa kuchangia na kuisapoti timu hiyo

Comments
Post a Comment