HEBU FAHAMU UNDANI HASA WA MGOGORO WA MALAWI NA TANZANIA JUU YA ZIWA NYASA
BLOG NO 1 TANZANIA !!


Je Unaufahamu Vizuri Mgogoro Uliopo Kati Ya Malawi Na Tanzania Juu Ya Ziwa Nyasa?
Kama hauufahamu au huwa unausikia juujuu tu basi leo nakuletea kwa undani zaidi.
Kama linavyofahamika kwa upande wa Tanzania kuwa linaitwa ziwa Nyasa na kwa upande wa Malawi wao wanaliita ziwa Malawi. Ni Ziwa la tatu kwa ukubwa Africa, lina ukubwa
wa kilometa za mraba zisizopungua elfu thelathini (30,000), pia lina utajiri wa maliasili nyingi sana ikiwemo;
1. Samaki wa aina zaidi ya 1000
2. Mafuta
3. Gesi
1. Samaki wa aina zaidi ya 1000
2. Mafuta
3. Gesi
Kuwemo kwa utajiri huo ktk ziwa Nyasa ambalo linaunganisha nchi Tatu, Tanzania, Malawi na Msumbiji kunapelekea wasiwasi kwa kila Nchi kutokana na shughuli zinazoendelea ktk ziwa hilo ambazo zinasemekana kufanyiwa maamuzi na nchi moja ambayo ni Malawi.
Vitu vikuu ambavyo inasemekana Malawi ameviruhusu ni pamoja na uchimbaji wa mafuta, gesi pamoja na uvuvi ndani ya ziwa Nyasa bila makubaliano na Tanzania, kitendo ambacho kinaifanya Tanzania iingiwe na hofu kubwa sio tu ktk maliasili zilizomo bali ktk usalama pia.
Malawi inasimamia makubaliano yaliyofanywa na wakoloni mnamo mwaka 1890 kwamba, Malawi ilikuwa chini ya utawala wa Mjerumani na Tanzania chini ya utawala wa Mwingereza na Mwingereza ndiye aliyeamua kuwa ziwa Nyasa lote ni mali ya upande wa Malawi ambako alikuwa anatawala Mjerumani na ndio sababu Malawi wanadai wanahaki ya kufanya wanachokitaka.

Tanzania, baada tu ya kupata uhuru chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwalimu aliibuka na kusema kwamba "Tunafahamu kuwa mipaka ya wakoloni inaonyesha kwamba ziwa Nyasa ni mali ya Malawi, hivyo tunawaomba wenzetu wapitie mipaka hiyo upya na ligawanywe kwa faida ya nchi zote zinazoguswa na ziwa Nyasa"
Mwalimu aliongea hayo miaka ya 60, akiwa na maana nzuri za kudumisha maelewano, amani, umoja, upendo, ushirikiano na mahusiano mazuri kati ya nchi zote zinazopakana na ziwa Nyasa. Hakuishia hapo alipeleka jambo hilo katika ngazi za Umoja wa mataifa ili lifanyiwe kazi.
Na kwa mujibu wa makubaliano mapya ngazi ya umoja wa mataifa ya Afrika ni kwamba kama kuna maziwa yanayo tenganisha nchi basi mipaka itapita katikati ya ziwa kwa maana ya Nusu kwa nchi moja na nusu kwa nchi nyingine, na iliwekwa wazi kwa mataifa yote na kufanyiwa kazi.

Licha ya makubaliano hayo Malawi hawakuridhika na waliona kama wameonewa ukiachilia mbali kwa wakati huu nchi hizi hazitawaliwi na wakoloni tena. Hivyo basi Malawi aliendeleza chokochoko za kudai kuwa ziwa Nyasa lote ni mali yake.
Kitendo hicho hakikuwafurahisha walio wengi, akiwemo aliyekuwa kiongozi wa Msumbiji Mh. Joachim Chissano ambaye alijaribu kumueleza Malawi na kumuomba akubaliane na makubaliano yaliyofikiwa ili nchi hizo ziwe na ushirikiano pamoja na mahusiano mazuri lakini hakufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Manamo mwaka 2014 Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Joachim Chissano (Msumbiji), Thabo Mbeki (South Africa) and Festus Mogae (Botswana), waliendelea kutoa ushauri kwa Malawi na kumkumbusha kuwa mipaka ya maziwa yote yaliyo zungukwa na nchi inapita katikati ya maji.

Licha ya Mh. Kikwete na viongozi wa Nchi Nyingine kukumbusha hayo aliongezea kwa kusema kwamba "inawezekana kabisa mambo haya kuzungumzika na kufikia muafaka bila kuingia kwenye vita"
Mimi binafsi niseme wazi tu "vita si nzuri na hakuna anayependa vita itokee na ninaamini Tanzania tumebarikiwa mioyo ya amani, si tu kwa wazee wetu bali hadi kwa vijana na hata watoto wanaozaliwa kila kukicha na ya kwamba hakuna kiongozi atakayekubali vita itokee", niwaase pia waTanzania wenzangu kokote mliko kuwa hakuna jambo linaloshindikana chini ya Mungu, tuombe sana sana mambo haya yafikie mwisho mzuri na tuendelee na maisha yetu ya kila siku.
Nirudi katika mgogoro huu, nikiangazia tatizo kubwa lililopo kwa wenzetu Malawi ambao wanahisi wakionekana wamekubali kuwa ziwa Nyasa liwe na mpaka katikati ya maji basi wataonekana wameshindwa kutetea mali yao kitu ambacho kinapelekea viongozi wa Malawi kuongea kauli za kichokozi.
Mfano, Chief Secretary wa Malawi Mr. George Mkondiwa anatamka na kuwaambia kuwa watu wa Malawi wasikubaliane na document au ramani zozote zitakazoonyeshwa na Tanzania au chombo chochote kwamba mpaka kati ya Malawi na Tanzania ktk ziwa Nyasa unapita katikati ya maji.

Kweli hili si jambo jema kwa kiongozi mkubwa kama Chief Secretary kwenye nchi. Na kupelekea Malawi kuchukua maamuzi yafuatayo ndani ya Ziwa Nyasa;
1. Malawi imeruhusu kampuni ya Hamra Oil ya United Arab Emirates kufanya utafiti ili kuchimba mafuta katika ziwa Nyasa bila kujali ukomo wa mipaka.
2. Malawi imeruhusu wavuvi kuvua samaki ktk ziwa Nyasa bila kujali mipaka.
3. Malawi inaendesha shughuli za utalii katika ziwa Nyasa bila kujali mipaka
4. Mnamo mwaka 2012 Malawi aliruhuru kampuni nyingine ya uchimbaji gesi na mafuta kuanza utafiti katika ziwa Nyasa, kampuni hiyo ya waingereza inajulikana kama Surestream
Pia inakumbushwaa, Mnamo mwaka 2012, Malawi chini ya uongozi wa Rais wake Joyce Banda ilijitoa ktk mazungumzo ya kufikia muafaka na Tanzania kwa madai ya kupeleka kesi kwenye International Court of Justice.
Chokochoko za Malawi kwa Tanzania zimekuwa ni zisizokwisha na zinaendelea licha ya Rais wake Peter Mutharika kuomba mkutano na Mh. Rais wa Tanzania wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Malawi Peter Mutharika alipoomba mkutano na Mh. Rais wa Tanzania wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli kipindi wamekutana ktk mkutano wa Umoja wa nchi huru za Afrika (AU) ili kujadili jambo hili kwa malengo ya kudumisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili, lakini kumetokea maneno mengine kupitia waziri wa mambo ya nje wa Malawi, nitakumwagia story chini kule.
Hivi Unaifahamu hii, pia inaweza kuwa miongoni mwa sintofahamu nyingi;
Kuna waTanzania wanane (8) walikamatwa Malawi ktk mgodi mmoja wa Uranium Disemba 2016 na kupewa kesi ya kwenda kufanya uchunguzi bila ruhusa toka kwa Serikali, sasa Malawi imewashikilia waTanzania hao ambao ni Ashura Yasiri (63), Wala-sa Mwasangu (30), Binto Ma-terinus (32), Christian Msoli (38), Martin Jodomusole (25), Layinali Kumba (47), Maliyu Mkobe (37) and Gilbert Ma-humdi (32).
Kuna waTanzania wanane (8) walikamatwa Malawi ktk mgodi mmoja wa Uranium Disemba 2016 na kupewa kesi ya kwenda kufanya uchunguzi bila ruhusa toka kwa Serikali, sasa Malawi imewashikilia waTanzania hao ambao ni Ashura Yasiri (63), Wala-sa Mwasangu (30), Binto Ma-terinus (32), Christian Msoli (38), Martin Jodomusole (25), Layinali Kumba (47), Maliyu Mkobe (37) and Gilbert Ma-humdi (32).
Mwaka huu 2017 mwezi wa kwanza Daily News iliripoti kuwa Tanzania inafanya juhudi za kidiplomasia na kuhakikisha waTanzania hao wanaachiwa, pia Daily News iliripoti kwamba Tanzania na Malawi zinafanya jitihada za ziada ili kukutana na kuzungumzia kwa undani mambo haya mawili.
1. Mgogoro juu ya mpaka wa ziwa Nyasa
2. WaTanzania waliokamatwa Malawi wakichunguza mgodi wa uchimbaji Uranium/Nuclear bila ruhusa ya Serikali
1. Mgogoro juu ya mpaka wa ziwa Nyasa
2. WaTanzania waliokamatwa Malawi wakichunguza mgodi wa uchimbaji Uranium/Nuclear bila ruhusa ya Serikali
Wakati juhudi hizo zikiendelea kuanzia Januari 2017 Yameibuka haya tena;
Mwezi huu wa tatu mwaka 2017, Rais wa Malawi amesikika akisema haya;
“Hebu tulilinde ziwa letu. Hili ni ziwa letu na ninaposema ziwa letu namaanisha ziwa lote. Mtu yeyote asifanye kosa la kubadili umiliki ambao umekuwepo kwa miaka 124 iliyopita,” alisema Mutharika akikaririwa na tovuti ya Nyasa Times ya Malawi juzi wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Nkopola Lakeshore mjini Mangochi Malawi.
Akiongeza kwa kusema;
“Tunathamini ziwa letu na tutahakikisha tunachukua hatua za kulilinda kwa gharama zozote,”
Ukiangalia kauli hizi za Rais wa Malawi ni tofauti na mazungumzo na Rais Wa Tanzania Dkt. Magufuli yaliyofanyika Januari 30 jijini Addis Ababa, Ethiopia wakati walipokuwa wakihudhuria kikao cha Umoja wa Afrika (AU). Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais baada ya kikao hicho, ilisema marais wote wameridhishwa na jitihada zinazofanywa na jopo la usuluhishi lililoteuliwa na Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).
Mimi Ninaomba nimalize zoezi langu kwa kukuacha ukijiuliza maswali yafuatayo kisha uniachie comment yako hapo chini;
1. Kwani Uganda na Kenya hazikutawaliwa na wakoloni? mbona wao hawakomalii ziwa Victoria kuwa la kwao lote?
2. Vipi kuhusu Kongo, kwani wao hawakutawaliwa na wakoloni? mbona wao hawakomalii ziwa Tanganyika kuwa ni lao lote?
3. Au wakoloni wao hawakuacha maagizo?
4. Au wao tu ndio wanapenda amani, upendo, na ushirikiano na Tanzania?
5. Kenya, Uganda, Kongo, Msumbiji, Malawi, Rwanda, na Burundi woote hao wanatuzunguka na wote walikwisha pigana vita na wengine kudiriki hata kupigana na kuchinjana wao kwa wao na hawalingani na Tanzania hata kidogo na kamwe hawawezi fikia amani na upendo tulionao waTanzania kwetu wenyewe na hata kwa wageni wetu, wewe kama Mtanzania unanini cha Kumshauri Malawi Juu Ya Hili?
;
Comments
Post a Comment