HII NDO RIPOTI YA KAMATI ALIYOUNDA NAPE ,HIKI NDICHO WALICHO KIGUNDUA MAZITO YAFICHUKA
BLOG NO 1 TANZANIA !!

RIPOTI YA KAMATI ILIYOUNDWA NA WAZIRI NAPE NNAUYE KUHUSU UVAMIZI WA MEDIA-
Waziri Nape Nnauye anapokea taarifa ya kamati aliyoiunda kuhusu uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds.
Tulifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds.-Balile
Tulifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa, tulimpigia simu lakini hakupokea.- Balile
“Hata tulipofika katika ofisi yake, aliondoka kupitia mlango wa nyuma”. -Balile
“Baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa”. -Balile
“Katika uchunguzi wetu, tumejiridhisha kuwa Mkuu wa Mkoa alivamia kituo cha Clouds akiwa anaendesha gari mwenyewe”. -Balile
“Kamati imejiridhisha kuwa RC na askari wenye silaha waliingia hadi ndani ya studio iliyokuwa ikirusha matangazo”. -Balile
“Kamati imejiridhisha pia kuwa palikuwa na vitisho kwa walinzi na wafanyakazi kwa kutumia askari wenye silaha”. -Balile
“Miongoni mwa vitisho ni kuwalazimisha kurusha kipindi vinginevyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya”. Balile
“Baada ya hapo aliwatisha kuwa yote yaliyotokea usiku ule, yabaki pale pale ndani” – Balile
“Tumejiridhisha kuwa RC Mkuu wa Mkoa aliingilia taratibu za uhariri kwa kulazimisha habari anayoitaka iruke” – Balile
“Kamati haikuona uthibitisho wowote kuwa kuna wafanyakazi waliopigwa na vitako vya bunduki au kupigwa mitama” – Balile
MAPENDEKEZO YA KAMATI
“Pendekezo la kwanza, Mkuu wa mkoa aombe radhi Clouds na kwa wanahabari wote” – Balile
“Pendekezo la pili, Waziri husika atoe taarifa kwa mamlaka husika ili Mkuu wa Mkoa achukuliwe hatua ” – Balile
“Pendekezo la 3, ni vyombo vya usalama kufanya uchunguzi juu ya askari kuingia Clouds na silaha za moto” – Balile
Comments
Post a Comment