HUYU NDIE TRUMP ATIA SAINI WENDAWAZIMU NA MACHIZI WAUZIWE BUNDUKI KAMA MTU MWINGINE YEYOTE!!

                                             BLOG NO 1 TANZANIA !!

Rais Donald Trump wa Marekani amesaini muswada wa kuondoa marufuku ya kununua silaha iliyokuwa imewekwa kwa watu wenye ulemavu mkubwa wa akili.

Muswada huo uliosainiwa na Rais wa Marekani ulipitishwa siku chache zilizopita na Baraza la Seneti kwa kura 57 dhidi ya 43 zilizoupinga.

Kusainiwa muswada huo kumetajwa kuwa sehemu ya orodha ya mwisho ya miswada mipya iliyosainiwa na Trump. Utiaji saini huo umefanyika katika Ikulu ya White House pasina kuhudhuriwa na mwandishi yeyote wa habari.

Silaha moto zinauzwa KAMA BIDHAA NYINGINEZO Marekani

Kulingana na sheria hiyo mpya, zaidi ya watu 750,000 wenye ulemavu wa akili ambao hawakuruhusika kununua silaha wakati wa utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Barack Obama, sasa wataweza kufanya hivyo kwa urahisi kabisa.

Serikali ya Obama ilikuwa imetoa agizo kwa Idara ya Usalama wa Jamii kuyapatia maduka ya uuzaji silaha orodha ya majina ya watu wenye ulemavu mkubwa wa akili wanaotaka kununua silaha.

Kurahisisha ununuzi wa silaha moto ni moja ya ahadi alizotoa Trump wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais.


Jumuiya ya Kitaifa ya Silaha (NRA) imeunga mkono KUPITISHWA SHERIA HIYO na kueleza kwamba si watu wote taahira wanahesabika kuwa ni makatili.

Maelfu huuawa kila mwaka Marekani katika matukio ya ufyatuaji risasi

Hata hivyo watetezi wa udhibiti wa umiliki silaha wanaamini kuwa kufutwa marufuku ya ununuzi silaha kwa watu wenye ulemavu wa akili kunaweza kuzidisha machafuko na vitendo vya ukatili unaohusiana na utumiaji silaha moto nchini Marekani...

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU