Kwa mujibu wa Frank Lampard hiki ndicho kikosi bora cha msimu cha ligi kuu England mpaka sasa
BLOG NO 1 TANZANIA !!


London, England.
GWIJI wa zamani wa Chelsea,Frank
Lampard,jana Jumatatu usiku kwenye kipindi cha Monday Night Football kinachorushwa na runinga ya SKY Sports alitakiwa ataje kikosi chake bora cha msimu cha ligi kuu England mpaka sasa wakati ligi hiyo pendwa ikiwa imebakiza miezi miwili ifikie mwisho.
Lampard,38,akiwa mgeni mwalikwa aliwaambia wenyeji wake David Jones na Jamie Carragher kuwa kikosi chake bora cha msimu mpaka sasa kiko kama ifuatavyo.
Kikosi Kamili
Kipa:David de Gea (Man Utd)
Mabeki:Cesar Azpilicueta
(Chelsea),Michael Keane (Burnley),David Luiz (Chelsea),Ryan Bertrand (Southampton)
Viungo:Adam Lallana (Liverpool), Dele Alli (Tottenham),N'Golo Kante (Chelsea),Eden Hazard (Chelsea)
Washambuliaji:Diego Costa (Chelsea),Harry Kane (Tottenham)

Comments
Post a Comment