MAKONDA AHAMIA CHANELI TEN AKITAKA AUNGWE MKONO BAADA YA KUHARIBU CLOUDS TV

                                                  BLOG NO 1 TANZANIA !!

Na Nizzoh Afrika Mwanaharakati.
___________________________

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amefanya ziara ya ghafla kwenye kituo cha runinga cha Channel ten kwa lengo la kutafuta kuungwa mkono na kituo hicho ikiwa ni pamoja na kupewa coverage ya matukio yake anayoyafanya. 

Makonda ambaye alifika kwenye ofisi za kituo hicho zilizopo mtaa wa Jamhuri na Zaramo akiwa na ulinzi mkali wa maafisa usalama wa taifa wengi waliokuwa wamevalia kiraia.


Ziara hiyo ilifanyika juzi siku ya ijumaa majira ya saa nane mchana. Katika hali isiyo ya kawaida makonda alisindikizwa na ulinzi mkubwa kuliko hata ule wa mawaziri. Idadi ya maafisa usalama ilitosha kujaa landcruiser mbili. Gavana huyo alikutana na mameneja wa idara mbalimbali za channel ten na ombi lake kuu likiwa nikuomba uhusiano mzuri na kituo hicho. 

Hata hivyo Taarifa za ndani zinadai kuwa uongozi wa kituo hicho ulishindwa kumpa jibu la moja kwa moja kwa kuhofia kutengwa na media zingine, jukwaa la wahariri pamoja na wananchi kwa ujumla hasa kutokana maazimio yaliyopitushwa juzi na vyombo vya habari kutokurusha ama kuandika habari yoyote ya Gavana huyo anaekabiliwa na tuhuma ya kughushi vyeti vya Elimu yake na matumizi mabaya ya madaraka.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU