MICHEZO MCHANGANYIKO ULAYA NA TANZANIA NIMEKUWEKEA HABARI ZOTE HAPA BONYEZA!!

                                           BLOG NO 1 TANZANIA !!

MADRID YARUDIA DOZI YA 3G KAMA MWANZO


Wakati Bayern Munich ikirudia dozi ya 5-1 kwa Arsenal, Real Madrid nayo imerudia dozi ya 3-1 kwa Nopoli na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya bao 6-2. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania, Real Madrid ilishinda 3-1 na Jumanne usiku ikafanya tena hivyo huko Italia kwa mabao ya Sergio Ramos dakika ya 51 kabla Dries Mertens hajajifunga dakika saba baadae huku Alvaro Morata akifunga la tatu katika dakika ya 90. Kwenye mchezo huo wa Champions League, Napoli ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 24 kupitia kwa Dries Mertens.
*****************************************************
MOURINHO AMCHINJIA BAHARINI RONEY


Wayne Rooney hajajumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United kilichosafiri kwenda Urusi kwa mchezo wa UEFA Europa League dhidi ya Rostov. Nahodha huyo wa Manchester United  si miongoni mwa wachezaji 20 waliochaguliwa na kocha Jose Mourinho kwaajili ya mchezo huo muhimu. Hata hivyo Rooney anaweza kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa robo fainali ya FA Cup Jumatatu usiku kufuatia kufungiwa kwa  Zlatan Ibrahimovic ambaye atakosa michezo mitatu ya michuano ya ndani ya England.
*****************************************************
ADHABU YA IBRAHMOVIC YAANZA  MECH YA CHELSEA

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ambaye amefungiwa kwa mechi tatu, ataanza kuitumikia adhabu hiyo katika mchezo wa FA Cup dhidi ya Chelsea Machi 13. Ibrahimovic amekumbana na adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko  Tyrone Mings wa Bournemotuh kwenye mchezo wa Premier League Jumamosi iliyopita. Mechi zingine atakazokosa Ibrahimovic  ni kati ya Middlesbrough Machi 19 na West Brom April moja. Michezo yote hiyo miwili ni ya Premier League. Ibrahimovic amekubali adhabu lakini Mings  ambaye naye alikabiliwa na adhabu kama hiyo kwa kumsigina kichwani Ibrahimovic amesema atakata rufaa, hatua ambayo mwisho wa siku inaweza ikamrefushia adhabu iwapo rufaa yake itatupwa.
*****************************************************

                  Chirwa aichakaza Kiluvya United

CHIRWA



Mshambuliaji Obrey Chirwa amefunga mabao manne akiiongoza Yanga kuichakaza Kiluvya United kwa mabao 6-1 na kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC).
Kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi, Yanga itakutana na Prisons katika mchezo wa robo fainali ambao haujapangiwa tarehe.

Chirwa alifunga mabao manne wakati mabao mengine ya Yanga yakifungwa na Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi.

Katika mchezo huo kocha George Lwandamina aliwaanzisha wachezaji wengi wa kikosi cha pili iliwachukua Yanga dakika 11 tu kuandika bao la kwanza lililofungwa na Mwashiuya baada ya kuwapiga chenga mabeki watatu wa Kiluvya na kutumbukiza mpira wavuni.

Dakika 31 Chirwa aliipatia Yanga bao la pili kwa shuti kali akimalizia pasi ya Mwashiuya kabla ya Edgar Mfumakule wa Kiluvya United kuifungia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya 40.

Chirwa aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya 45 baada ya kumfinya beki wa Kiluvya kisha kuachia shuti lililogonga mwamba na kutinga wavuni akimaliza kazi safi ya Juma Mahadhi kabla ya kufunga tena bao la nne dakika ya 70.

Mahadhi aliipatia Yanga bao la tano dakika ya 74 kwa shuti kali nje kidogo ya 18, lakini baada ya bao hilo aliumia na hakurejea tena uwanjani hivyo kuwafanya Yanga kucheza pungufu mpaka mwisho wa mchezo.

Chirwa alikuwa mwiba mkali kwa Kiluvya United alihitimisha karama ya mabao kwa Yanga baada ya kufunga bao la sita kwa shuti kali akimalizia krosi safi ya Saimon Msuva.

Katika ratiba hiyo inaonyesha vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba imepangwa kucheza na Madini ya Arusha wakati Azam FC itakuwa na kibarua kizito mbele ya Ndanda, wakati Kagera Sugar itacheza dhidi ya Mbao.

Mshindi wa kombe hilo atajinyakulia kitita cha Sh. 50 milioni na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
*****************************************************
    HATIMAYE AFRICAN LYON YAWEKWA SOKONI



IMEBAINIKA kuwa timu ya African Lyon ambayo imerejea Ligi Kuu Tanzania Bara imewekwa sokoni akitafutwa mnunuzi mwenye mkwanja wa kutosha. Ingawa mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangenzi “Zamunda” amekanusha kuiuza akisema wanataka kuimarisha uwekezaji, lakini ukweli ni kuwa anaipiga bei timu hiyo. Imeelezwa kuwa gharama kubwa za kuendesha timu bila ya kuwa na uzalisahaji wa kutosha ndio unaomsukuma kuiuza timu hiyo. Kwa sasa mazungumzo baina ya African Lyon na kampuni ya GSM Limited yanaelekea kukamilika. African Lyon iliuzwa mwaka 2010 na mfanyabiashara anayetaka kumiliki hisa nyingi ndani ya Simba SC, Mohammed Dewji “Mo”, ambaye pia aliinunua mwaka 2007 kutoka kwa wafanyabiashara wa soko la Mbagala, wakati huo ikiitwa “Mbagala Market”. 


Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU