MJANE ALIYEPEWA ULINZI NA RAIS MAGUFULI ABURUZWA KORTINI KWA KESI YA DAWA ZA KULEVYA
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha mbele ya Rais Magufuli kuwa ni Swabaha Mohamed na kudai kwamba yeye ni mjane wa marehemu Mohamed Shosi kutoka Tanga ameburuzwa mahakamani na Saburia Soshi baada ya kumtuhumu kuwa anajihusisha na dawa za kulevya na kudai kuwa anazo picha zake.
Swabaha aliyasema hayo mbele ya Rais Magufuli ambapo alidai Saburia ambaye ni mtoto wa mke mwenzake amekuwa akimtishia maisha kwa kutaka kumuua na kwamba anajihusisha na dawa za kulevya.
Mama huyo aliomba ulinzi kwa rais kwa madai kuwa amekuwa akitumia jumbe za vitisho na watu wanaotaka kumdhulumu mirathi ya mumewe akiwemo mtoto huyo.
Rais Magufuli alimuagiza IGP Mangu kuhakikisha mama huyo anapewa ulinzi na pia viongozi wa mahakama wahakikishe kesi hiyo ya mirathi inashughulikiwa haraka ili haki iweze kupatikana.
Saburia amemburuza mama huyo mahakamani kufuatia kauli yake huku akiitaka mahakama itamke kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake ni kashfa. Mbali na hilo, mlalamikaji anaiomba mahakama imuamuru Swabaha amlipe TZS milioni 400 ikiwa ni gharama za madhara aliyoyapata kwa kashfa hiyo, riba pamoja na gharama za kuendesha kesi.
Saburia amekanusha kuwa hakuwahi kuhusika kwa namna yoyote ile na biashara ya dawa za kulevya na kwamba taarifa hiyo ilitolewa kwa lengo la kumchafua.
Ngudu wengine wa Mohamed Shosi wamekuwa wakisema kuwa mwanamke huyo aliyekwenda mbele ya rais ni muongo na kuwa si mke halali wa marehemu licha ya yeye kudai kuwa anacho cheti halali cha ndoa.

Comments
Post a Comment