PLUIJIM AKANUSHA TAARIFA ZA KUJIUNGA NA SINGIDA UNITED
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Aliekua Kocha na mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Hans van der Pluijm amekanusha kusaini mkataba kuifundisha timu ya Singida United iliyopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao.
Aliekua Kocha na mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Hans van der Pluijm amekanusha kusaini mkataba kuifundisha timu ya Singida United iliyopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao.
Akiongea na Clouds fm kupitia kipindi cha Sports Extra Pluijm amesema hajasaini mkataba wa kuifundisha Singida United kama taarifa zinavyoenea kwenye mitandao ya kijamii lakini amesema ana offer tatu mkononi na atatoa taarifa baada ya kufanya uamuzi ni wapi anaelekea kati ya hizo klabu tatu zilizoonesha kuhitaji huduma yake...“Sijasaini mkataba mahali popote na timu yoyote lebda kesho mchna (leo) halafu jioni ninaweza kukutaarifu nitakwenda kufundisha wapi.”
“Kuna picha kwenye mitandao ya kijamii nikionekana nikiwa na kijana wa Zimbabwe ambaye ni rafikiangu wa muda mrefu, alipita nyumbani kwangu na kuniomba niongozane nae anapokwenda kwenye timu yake.”
“Kijana huyo ni rafiki wa Chirwa pia, nina offer tatu lakini bado sijafanya maamuzi naenda wapi, kesho (leo) nitakuwa nimeshajua naelekea wapi na kila mtu atajua napokwenda baada ya kufanya maamuzi.”Alisema pluijm
Comments
Post a Comment