Rais Magufuli aamuru kushikiliwa kwa hati za kusafiria za mkandarasi wa India

                                            BLOG NO 1 TANZANIA !!


Rais Magufuli aamuru kushikiliwa kwa hati za kusafiria za mkandarasi wa India


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameagiza kushikiliwa kwa hati za kusafiria za mwakilishi wa kampuni ya ukandarasi ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya nchini India, Rajendra Kumar, hadi kampuni hiyo itakapokamilisha mradi wa maji wa Ng’apa Lindi Mjini.
Mbali na Kumar, amri hiyo ya Rais Magufuli inawahusu vile vile wasaidizi wake. Mradi huo chini ya kampuni hiyo ulipaswa kukamilika takriban miaka miwili iliyopita, yaani Machi 17, 2015.
Rais Magufuli ambaye yuko katika ziara mikoa ya kusini, alitoa agizo hilo leo – Machi 3, 2017, alipotembelea mradi huo ambao unatarajiwa kuzalisha zaidi ya lita za ujazo milioni tano za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa mji wa Lindi ambao, kwa muda mrefu, wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa maji.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu leo, Magufuli amesikitishwa na usimamizi mbovu wa mradi huo ambao umekwishapatiwa shilingi bilioni 21.8 kati ya shilingi bilioni 29 zilizopangwa kutumika hadi kukamilika kwa mradi huo, akionya kwamba, endapo mradi huo hautakamilika katika muda wa miezi minne kuanzia sasa atachukua hatua kali zaidi.
“Ikipita miezi minne nisilaumiwe, hatuwezi kukubali wananchi wa Lindi wanashida ya maji, fedha zimetolewa, mkandarasi anaamua fedha India, mradi umecheleweshwa kwa miaka miwili na mkandarasi hayupo kwenye eneo la ujenzi halafu mnaopaswa kusimamia mnamuangalia tu wakati sheria zipo, kwa nini hamkufukuza muda wote?” alihoji Magufuli
Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji mhandisi Gerson Lwenge alisema mradi huo unatekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) na Jumuiya ya Ulaya (EU) na hadi sasa, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 85 na kwamba mkandarasi amesimamisha kazi kutokana na kuishiwa fedha

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU