Sergio Ramos aipeleka Real Madrid kileleni La Liga
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Madrid,Hispania.
NAHODHA Sergio Ramos (pichani) akishangila baada ya kuifungia Real Madrid bao la pili katika ushindi wa mabao 2-1 nyumbani Santiago Bernabeu dhidi ya wabishi Real Betis.
Wegeni Real Betis ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Antonio Sanabria kufunga akitumia vyema makosa ya kipa wa Real Madrid,Keylor Navas na kutumbukiza mpira kimiani.Navas nusuru aonyeshwe kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Darko Brasanac.
Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kusawazisha Real Madrid akiunganisha vyema krosi ya Marcelo na kuandika bao lake la 26 la msimu kabla ya Sergio Ramos kufunga bao la ushindi.
Ushindi huo umeipeleka Real Madrid kileleni mwa msimamo wa ligi ya La Liga baada ya kufikisha pointi 62.Pointi mbili mbele ya Barcelona yenye pointu 60.Ikumbukwe Real Madrid ina mchezo mmoja pungufu.


Comments
Post a Comment