SOMA!! ALICHOKIONGEA RUGE MWANZO-MWISHO UVAMIZI ULIOTOKEA KWENYE OFISI ZA CLOUDS MEDIA
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Kufuatia habari mbalimbali kuhusu Clouds Media Group kuhusiana na tukio la kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Zifuatazo ni sentensi za Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Bw. Ruge Mutahaba wakati akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360:
Alhamisi asubuhi tulikuwa na kikao na Kamati ya Maudhui ya TCRA kutupatia msasa kidogo. Katikati ya kikao Makonda alitutembelea tukaongea mambo kadhaa tukaagana na watu wa TCRA Wakati natoka ofisini nje nilikutana na Makonda na Vijana wa Shilawadu nikauliza kwema hapa nikajibiwa ni Story za kawaida tu. Nikiwa kwenye Gari alinifata mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kuniambia kuhusu mwanamke aliyezaa na mchungaji. Nikawauliza hiyo Story mna uhakika nayo kwenye balance mtampata Mchungaji Gwajima? nilimpigia Kerry kumuuliza hii story! Nilitoa maelezo kwa boss wa vipindi Clouds TV kuhusu hiyo Story isiyokuwa na maana sababu haina balance kuwa isiruke hewani. Mida ya Saa 10 Alhamisi nilipata Simu ya Gwajima kunieleza kuhusu kuwepo kwa habari inayonihusu nikamueleza hiyo Story haitoruka. Nilimueleza Boss Kerry awasiliane na Makonda kwamba video yake haitoruka hewani sababu haina balance. Siku ya Ijumaa Saa tano kasoro nilipokea Simu kutoka kwa HR wetu mkuu wa mkoa ameingia ofisini akiwa na Askari sita wenye silaha. Baadaye nilipata Simu kutoka kwa Mkurugenzi Joseph Kusaga kwamba anatupiwa lawama na mkuu wa mkoa amezuia kipindi chake. Baadaye nikampigia Simu Makonda nikamuuliza kwanini hakunipigia Simu mimi kwanza kabla ya kufanya lile jambo. Nilimuagiza Sam ambaye alikuwepo mapokezi alinieleza Mh Makonda alikuwa anachukua kitu kwenye flash. Kwa Mara ya kwanza Makonda anatuvunjia heshima sisi kama Rafiki zake tulifanya kazi naye Uzuri tangu akiwa Mkuu wa wilaya. Ukweli sisi kama chombo cha Habari lazima tujenge heshima ya kutoa habari zenye uwiano lazima tuiheshimu taasisi yetu. Hofu yangu ni kwamba kama mimi nipo na mkurugenzi yupo kwanini asingetengeneza mazingira ya kuonana na sisi kwanza. Naomba nieleweke wazi hatuwezi kumuacha mtu akatupanda kichwani hii ni dharau kwangu nasimamia watu 200 asinidharau. Panapotokea misingi ya hofu lazima tuweke wazi kabisa bila kificho panopohitaji ukweli lazima tuweke wazi ukweli usemwe. Mfano wangu ni kwa Simba na Yanga ni mahasama lakini chombo kinachowasimamia kikiingilia maslahi yao wanaungana. Nimefurahi wanaoitwa mahasimu wetu Majey alitupigia simu, Reginald Mengi atafika leo kututembelea Tasnia ya Uhuru wa habari lazima ilindwe. Mimi sitaki kuona bunduki mtaani kwa maslahi ya Vizazi vya kesho bunduki ziwepo wanapolinda benki sio kwenye media. Tuhukumiwe kama Taasisi napenda Vijana wapende kutengeneza kesho yao kwa Uhuru lakini kwa chuki za kupandikizwa na watu Vijana wa SHILAWADU wapo kwenye hofu wametishwa wamepoteza morali na kazi yao hawana Amani tena wameomba likizo. Sisi tunampenda Makonda hatulipi chochote tunaipenda Dar es Salaam tulifanya kampeni ya Dar Mpya kwa Mapenzi yetu wenyewe. Sakata hili lisihusishwe na kutetea vita dhidi ya madawa ya kulevya kama mtu kakosea ni kakosea tu kwa utashi wake. Sisi tuna namna yetu ya kuadhibiwa tunahitaji kuwe na Uhuru wa habari, sio kwakua una mamlaka ya eneo fulani ukatupanda kichwani. Viongozi wetu wanapenda kumtaja Mungu lakini matendo yao ni tofauti watu wanaumia kwenye hili. Tukiongea kwa watu wanasema tunahitaji mtu atumbuliwe lakini sisi tunaongea kwa nafasi yetu tumeumia kwenye hili.

Comments
Post a Comment