TORRES AUNUSURIKA KUFA UWANJANI, AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUANGUKIA KICHWA VIBAYA

                                           BLOG NO 1 TANZANIA !!



MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana alikimbizwa hospitali
 nchini Hispania baada ya kuumia kichwani. Torres aliuamia
 baada ya kuingia dakika ya 65 akitokea benchi kuchukua
 nafasi ya Kevin Gameiro.Mshambuliaji huyo wa zamani wa
 Liverpool na Chelsea, kwanza aliumia mapema tu katika 
mchezo wa Liga usiku wa jana dhidi ya Deportivo La Coruna
 Uwanja wa Manispaa ya Riazor mjini La Coruna, timu hizo
 zikitoka sare ya 1-1.Aliangukia kichwa uwanjani baada ya
 kugongana na Alex Bergantinos na kuwashitua wachezaji
 wenzake baada ya hali yake kubadilika. Gabi alipigwa na
 Torres wakati akijaribu kumzuiaa asiueze ulimi.Wachezaji wa
 Atletico Madrid wakijaribu kumzuia Fernando Torres
 asiumeze ulimi baada ya kuumia jana, Hata hivyo, Atletico
 Madrid imethibitisha mchezaji wake huyo anaendelea vizuri
 hospital. Katika mchezo huo, Florin Andone alianza
 kuwafungia wenyeji dakika ya 13, kabla ya Antoine
 Griezmann kuisawazishia Atletico dakika ya 68.Baadaye
 Torres mwenyewe akaandika kwenye akaunti yake Twitter
 kuwaambia mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya hali yake:
 "Asante nyingi kwa wote kwa kunifuatilia hali yangu na kwa
 meseji zenu za kunifariji. Ilikuwa ni hofu tu. Natumai kurejea
 karibuni!,"

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU