Askari Polisi watatu wauawa na majambazi Mkuranga

                                               BLOG NO 1 TANZANIA !!
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi watatu wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU