BREAKING NEWS:KILOMBELO WANANCHI WAVUNJA MLANGO WA KITUO CHA POLISI NA KUWATOA WATUHUMIWA NA KUWAUWA LEO HII

                                              BLOG NO 1 TANZANIA !!
picha maktaba
Na muandishi wetu Jumbe Musa
kutoka Chita-Kilombero, watu watatu wameuawa na wanachi wenye hasira baada ya kufanya mauaji juzi ucku ya kumuua mwanamke na kumtoa baadhi ya viungo vya uzazi, wamedai kuna mtu huwa anatuma na kupewa pesa, hao watuhumiwa ni wakazi na wenyeji wa Mbeya, wameuawa leo asubuhi majira ya saa tatu, kwani maaskari waliwashikilia hapo kituoni locapu na lengo lilikuwa kuwasafirisha kuwaleta Ifakara mjini kituo kikubwa, lakini baada ya treni hiyo kufika hapo Chita station wananchi waligoma watuhumiwa hao kusafirishwa, kwenye treni hiyo maarufu kwa jina la kipisi inayofanya safari zake kuanzia Makambako-Mlimba na kuishia mkamba(RUAHA)..
ndipo wananchi wakaenda kituoni na kuvunja mlango wa kituo cha polisi na kuwatoa watuhumiwa hao watatu na kuwashughuhulikia kwa kuwapga hadi kuwaua... wanachi wanadai wamechoshwa na matukio hayo ambayo utokea mara kwa mara, na kudai once wanapopelekwa polisi baada ya muda huachiwa... watuhumiwa hao wamedai huwa wanatumwa na mtu huko mbeya kupeleka viungo hivyo...

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU