Habari za michezo zote nimekuwekea hapa: Matokeo ya jana,usajili,mgomo Yanga,na habari nyingi za kimichezo
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Arsenal yairejesha Man United nafasi ya sita England
Arsenal yairejesha Man United nafasi ya sita England
London, England.
ARSENAL imefanikiwa kuirejesha Manchester United mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ya England baada ya usiku huu kuifunga West Ham United kwa jumla ya mabao 3-0 nyumbani Emirates.
Arsenal ambayo ilikuwa haijaonja radha ya ushindi kwenye ligi kuu tangu Februari 11 imejipatia mabao hayo katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa Mesut Ozil 58', Theo Walcott 68' na Olivier Giroud 83'.Kipindi cha kwanza hakikushuhudia bao.
Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 54 na kushika nafasi ya tano ambayo hapo awali ilikuwa inashikwa na Manchester United ambayo sasa imeporomoka mpaka nafasi ya sita kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Alichokisema Mkwasa baada ya wachezaji Yanga SC kudaiwa kutaka kugoma
KATIBU MKUU wa Yanga SC,Charles Mkwasa amewataka wachezaji wa klabu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha mdororo wa kiuchumi kinachoikumba miamba hiyo ya soka nchini.
Mkwasa ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa wachezaji wa klabu hiyo wanataka kugomea mchezo wao wa Jumamosi wa Jumamosi wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger kwa madai ya mishahara yao.
Akiongea na kituo kimoja cha redio cha jijini hapa,Mkwasa ambaye kwa sasa yuko mkoani Morogoro alikokwenda kuhudhuria msiba wa kaka yake amekiri kweli Yanga SC inadaiwa mishahara na wachezaji wake lakini amesema kama kweli wachezaji hao wataamua kugoma kwa madai ya mshahara wa mwezi mmoja basi watakuwa wanakosea sana.
Mkwasa ameongeza kuwa uongozi wa Yanga SC unafahamu kuwepo kwa deni hilo lakini amewataka wachezaji kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Jumamosi katika kipindi hiki ambapo uongozi unapambana kwa kila hali kupata fedha ili kuwalipa mishahara na madai yao mengine yanayofikia Milioni 400.
"Ni kweli wachezaji wanadai mishahara yao pamoja na malimbikizo yao mengine ya nyuma.Uongozi unapambana kuhakikisha unapata fedha kwa ajili ya kulipa deni hilo.Tutalipa muda si mrefu,tayari tumeshaongea na wanachama pamoja na wadau mbalimbali ili watusaidie.Pia tumeshafanya mawasiliano na bodi ya ligi ambayo tunaidai malimbikizo ya fedha za haki za matangazo ya televisheni.Alisema Mkwasa.
Messi aiongoza Barcelona kuifumua 3-0 Sevilla
Barcelona, Hispania.
LIONEL Messi (Pichani) ametengeneza bao moja,amefunga mabao mawili na kuiwezesha Barcelona kuifunga Sevilla mabao 3-0 katika mchezo safi wa ligi ya La Liga ulioisha hivi punde huko dimbani Camp Nou jijini Barcelona.
Messi ambaye alikosa mchezo wa Jumamosi iliopita dhidi ya Granada kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja ameandikisha mabao yake katika dakika za 28 na 33. huku lile Luis Suarez
Ushindi huo umeifanya Barcelona ifikishe pointi 69 na kukalia kwa muda kiti cha uongozi ligi ya La Liga kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya wapinzani Real Madrid wenye pointi 68
68 na michezo miwili mkononi.Baadae Real Madrid watashuka dimbani kucheza na Leganes na ikiwa watashinda mchezo huo wakarejea kileleni.
Sevilla ambao walilazimika kumaliza wa leo wakiwa wakiwa na wachezaji kumi (10) baada ya kiungo wake,Machín Pérez Vitolo kutolewa uwanjani kwa kadi mbili za njano wako nafasi ya nne wakiwa na pointi 58.
Bila Ronaldo,Bale Real Madrid moto tu,yashinda 4-2 ugenini
Leganes,Hispania.
IKICHEZA bila ya nyota wake wawili,Cristiano Ronaldo na Gareth Bale waliopumzishwa kwa sababu mbalimbali,Real Madrid Jumatano usiku imepata ushindi mnono wa mabao 4-2 ugenini Butarque dhidi ya wenyeji wao Leganes katika muendelezo wa michezo ya ligi ya La Liga.
Alvaro Morata ndiye aliyekuwa nyota wa Real Madrid kwenye mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za 18 na 23.Bao la tatu limefungwa na James Rodriguez dakika ya 15 huku bao la nne likifungwa dakika ya 48 na beki Martin Mantovani aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.
Mabao ya wenyeji Leganes yamefungwa na Gabriel Appelt Pires dakika ya 32 pamoja na Luciano dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza.Mabao hayo yameifanya Real Madrid ifikishe pointi 71 na kurejea nafasi ya kwanza La Liga, pointi mbili mbele ya Barcelona yenye pointi 69.
Thiery Henry: aponda kiwango cha ozil cha sasa
Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thiery Henry amemtuhumu Mesut Ozil kutokana na kucheza kivivu uwanjani.
Baada ya Arsenal kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Manchester City siku ya Jumapili, Henry alisema kuwa mchezaji huyo asingeweza kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal cha zamani kwa kiwango alichonacho baada ya mechi . “Anacheza vizuri sana, na mwaka jana kila mtu alikuwa akimsifu,” Henry ameiambia Sky Sports.
“Anapocheza ndani ya fulana ya Arsenal, wakati mwingine hachezi katika kiwango cha Arsenal. Namkubali sana na jinsi anavyocheza, lakini kama angekuwa kwenye timu yangu ya zamani, najua kulikuwa na wakali ambao wangemkabili na huenda ndicho anachohitaji,” ameongeza.
“Katika timu yangu ya zamani, kila mmoja alikuwa na fursa ya kuongea. Sylvain Wiltord aliongea. Edu kadhalika. Hata Nwankwo Kanu alikuwa na ya kusema. Jens Lehmann, alikuwa akiongea muda wote. Ni lazima ucheze kweli.”





Comments
Post a Comment