HII INATISHA:UNICEF: Watoto 269 walio chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku Tanzania
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema kuwa, jumla ya watoto 269 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku nchini Tanzania.
Hayo yalisemwa leo na mwakilishi wa (UNICEF) nchini Tanzania Maniza Zaman kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri (TEF) huko mjini Moshi.
Aidha ameongeza kuwa, jumla ya wajawazito 556 hufariki dunia pia kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi ndani ya taifa hilo, suala linalotishia maisha ya akina mama.
Zaman amesema kuwa, kwa mujibu wa utafiti walioufanya kuhusiana na masuala ya elimu kwa watoto, ni asilimia 39 tu ya watoto wa kike na kiume ndio wanaohitimu elimu ya sekondari nchini humo kila mwaka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika uwanja huo.
Maniza Zaman ameitaka serikali kushirikiana na asasi mbalimbali za kujitegemea kuwekeza katika masuala ya watoto hususan katika sekta za elimu na huduma bora za afya ili kuepusha vifo vya watoto wadogo.
Chanzo: parstoday.com
Comments
Post a Comment