HII SASA TO MUCH: UONGOZI WA UWANJA WA CCM KIRUMBA UMELALAMIKA MASHABIKI WA SIMBA KUHARIBU UWANJA WAO

                                            BLOG NO 1 TANZANIA !!

Mwandishi Wetu,Mwanza.

Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba, kupitia Meneja wa Uwanja Ndugu Steven E. Shija unapenda kutoa taarifa za uharibifu wa Uwanja.

Mechi iliyochezwa Tarehe 10.04.2017, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya Mbao FC Vs Simba SC umesababisha uharibifu Mkubwa kwenye Maeneo ya kuingilia Wachezaji, Waamuzi na Geti Namba 4 ambapo walikuwa wamekaa Mashabiki wa Simba

Uharibifu huo umetokana na Mashabiki wa Timu ya Simba SC kupanda Juu ya maeneo ya Kivuli yaliyojengwa kwenye maeneo yaliyotajwa ( Vyumba vya Kubadirishia Nguo kwa wachezaji, Waamuzi na Geti namba Nne), uharibifu huo umepelekea kushindwa kufunga Milango ya Mbele ambapo ni hatari kwa usalama wa maeneo hayo muhimu


Hivyo uongozi wa Uwanja umeishazitaarifu Mamlaka husika ili zichukue hatua kwa Wanaohusika ili kuhakikisha eneo hilo linatengenezwa mapema kabla ya Mechi ya Toto African Vs Simba SC Tarehe 15.04.2017 

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU