KUTANA NA MBUNGE WA CCM ANAEOGOPA KUJA DAR BAADA YA KUGOMBANA NA MAKONDA ASEMA AMEI MISS MNO DAR
BLOG NO 1 TANZANIA !!


Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillaly amesema yeye ni mmojawapo wa wabunge waliotishwa na Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Amesema hayo leo wakati akichangia hotuba ya bajeti waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2017/18.
Amesema yuko tayari kutoa ushahidi ukihitajika na kwamba anaogopa kwenda mkoa huo hivi sasa ingawa anapatamani.
Nukuu za Wabunge jana:
“Nipo tayari kuthibitisha kwamba waliovamia Clouds Tv ni Usalama wa Taifa kutoka kikosi cha Ulinzi wa Rais, Nipo tayari pia kuthibitisha aliyemtoloea bastola Nape ni Usalama wa Taifa” Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo)
“Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No!” Juma Nkamia (CCM)
“Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi)”. Hussein Bashe (CCM)
Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu” Ridhiwani Kikwete (CCM)
Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana” Hillary Aeshi (CCM)
Tafakari, Chukua hatua
Comments
Post a Comment