LEO NI ZAMU YA FAMILIA YA ROMA,YA BEN SAA NANE WAO WAMESHALIA VYA KUTOSHA JE HUWEZI JUA KESHO NI ZAMU YA FAMILIA YAKO KU LIA JUU YAKO?
BLOG NO 1 TANZANIA !!
Leo zamu ya mtoto wa Roma hajui baba yake yuko wapi yuko hai au ameuwawa leo mke wa Roma analia hajui hali ya mumewe huko alipo ana hali gani kama ni kukamatwa si angekamatwa hata afungwe pingu apelekwe polisi lakini kuvamia studio na kumteka na kumpeleka kusiko julikana hii sasa inazidi kututisha zaidi huu mfumo wa kuteka na kuficha watu sasa umeshakua maarufu Tanzania leo ni ROMA na familia yake wanalia Familia ya kina Ben saa nane wao mpaka sasa bado wana maruerue hawaelewi bora yule Dada wa Moshi yeye maskini alitekwa sasa hivi yuko chini ya ardhi maana ye kaonekana akiwa amefariki wengi wamekua wakipotea katika hali ambayo haieleweki ni jukumu la serikali yetu tuliyoipa mamlaka ya kutulinda ituhakikishie usalama wetu leo wale kesho wewe na familia yako mwalimu Nyerere alishawahi kutoa mfano mmoja kua mfano waislamu wakiwatenga wakristo wakawauwa watawauwa mwisho wataisha wakiisha wataanza kuuana wenyewe sasa watatekwa kina Roma tutatekwa sisi atatekwa mumeo au mwanao au kaka yako ndio siku na wewe utajifanya kusimama kulaani lakini itakua umeshachelewa sababu tabia itakua imeshaota mvi kwa hio haitawezekana kurekebishwa ni jukumu letu wote kupiga makelel sasa kua hili linatisha na kwanini iwe kipindi hiki? MUNGU iangalie Tanzania uliyotupa inapokwenda Shusha mkono wako wa Rehema kwa watu wako walinde haribu mipango ya kuipaka doa Tanzania yako tumezoea Amani tumezoea upendo maswala ya kutekana kuuana na kutishiana tulikua tunayaona kwenye video
GK HIM SELF!!

Comments
Post a Comment