Ofisa wa Polisi mwingine auawa Kinyerezi

                       
                  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni 



Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala.
  
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake.

Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni.
Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye.
“Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

MWANJALE AONGEZEWA SIKU NYINGIZE ZA MATIBABU

Hii hapa ratiba ya michuano yote mikubwa ya leo hii,Shirikisho,Epl,La Liga,Bundesliga na Seria A