Posts

Showing posts from August, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya August 17

Image

Zambia: Kuanzia Sasa Kila Mwananchi ni Lazima Apimwe UKIMWI, Sio Hiari Tena

Image
Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba. Rais Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya serikali ya kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.

Mtoto Mchanga wa Miezi 6 Aliyejeruhiwa na Polisi Afariki Dunia

Image
Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na familia yake. Samantha Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu.

Umoja wa Mataifa Wakataa Ombi la Raila Odinga

Image
Afisa wa Umoja wa Mataifa, amekataa ombi la kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga la kutaka umoja huo kufanya tathmini mpya ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, ameunga mkono kauli ya Katibu Mkuu, Antonio Gutrres, ya kuwataka wanasiasa wa Kenya wanaopinga matokeo ya uchaguzi kufikisha masuala hayo mbele ya taasisi zenye mamlaka ya kutoa maamuzi Kikatiba.

Mwanaume Amuua Mpenzi Wake Kisha na Yeye Kujiua Dar

Image
Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Pius amezikwa leo makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa baada ya mpenzi wake kumuua kwa kumpiga na kitu chenye nchi kali kisha mwili wake kuutupa kwenye shamba huko Chanika jijini Dar es Salaam.

HATIMAYE JUKWAA LA WAHARIRI WAANZA KUMEGUKA,MMOJA WAO AKILI WAMEJICHANGANYA KATIKA MKUTANO NA RC MAKONDA

Image

Jeshi la Polisi limewaua wahalifu 13 Kibiti na kutwaa bunduki nane

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha  8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro akionesha makasha ya risasi(magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa ya kitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) MussaAlli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katikat ukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti. Mkuu wa Jeshi la Po...

Rais Museveni abadilisha tarehe yake wa kuzaliwa

Image
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni. Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena. Lakini nadhari nyingine imeibuka  ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70. Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena katika awamu ya sita. Museveni alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awa...

Mahakama Yatoa ONYO la Mwisho kwa Tundu Lissu

Image
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo. Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani. Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Ntobesya amedai kuwa mteja wake ana udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika. Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo  ameahirisha kesi hiyo hadi August 14/2017. Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam.