MBUNGE wa Kwimba, Mwanza, Shannif Mansour (CCM), anatuhumiwa kugoma kulipa kodi ya eneo lake la ardhi lenye ukubwa wa hekta 39,000, kiasi cha zaidi ya Sh. 500 milioni tangu mwaka 2010. Mansour kupitia kampuni yake ya Sineji Tanzania Limited, anatuhumiwa kuigomea serikali kulipa kiasi hicho cha fedha kwa madai yeye hawezi kulipa fedha hizo kwa kuwa anafahamiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi. Eneo hilo la Mansour na kampuni yake inayojihusisha na utengenezaji wa malighafi za ujenzi ikiwemo kusaga kokoto, lililopo kata ya Buhongwa, Nyamagana pia baadhi ya wananchi wanalalamika kulaghaiwa fedha za fidia za maeneo yao.